HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 12, 2025

Sheria Zinazosikiliza Wananchi: Tume ya Haki za Binadamu Yatambua Juhudi za OCPD

 


 Na: Calvin Edward Gwabara – Dar es salaam.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Bwana Nyanda Shuli amepongeza Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria OCPD kwa kufanyia kazi mapendekezo ya mabadiliko ya sheria mbalimbali za nchi ambayo yanaibuliwa na Wananchi kwenye maeneo mbalimbali.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Bwana Nyanda Shuli  akipata maelezo kutoka kwa Bi Happyphania Luena kutoka OCPD.

Pongezi hizo amezitoa wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara SABASABA yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

“Ofisi hii inatoa huduma ambazo zinaelekeana sana na zetu, maana sisi tunapokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau na wananchi kuhusu sheria zetu nchini na baadae zinapitia michakato mbalimbali lakini mwisho wa siku lazima zipite kwenu kwaajili ya kuandika na kuzifanyia mabadiliko kabla ya kupelekwa bungeni ili zipitishwe, na kwa maana hiyo tunashirikiana katika kuwezesha haki na sheria zinakwenda na wakati” alifafanua Kamishna Shuli.

Aliongeza “Kuna kipindi tulienda Mikoa ya kusini kwenye uchunguzi fulani, tukakutana na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Kusini akatuambia jamani tusaidieni kwani kuna sheria tunazitumia hapa lakini ukizitazama tunaona kwa mazingira ya utungwaji wake na mazingira yetu zimeenda zaidi wakiitaja sheria ya Uhujumu uchumi inagusa kwato za swala na pembe za digidigi kuwa ni uhujumu uchumi lakini tunaona kipindi kile sheria ililenga kulinda wale wanyama “ Big 5” wasipotee lakini sheria ikaingiza swala na digidigi na sasa tuna watu wengi Magereza kwa kesi hizo na hawapewi dhamana” .

Kamishna Shuli amesema anashukuru baada ya mchakato mrefu wa maoni hayo sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko na kuiweka kulingana na matakwa halisi ya malengo ya serikali kwa maslahi mapana ya taifa tofauti na ilivyokuwa awali na hapo ndipo unapoonekana umuhimu mkubwa wa Ofisi hii lakini pia ushirikiano uliopo katika utekelezaji majukumu.

Kwa upande wake Mwandishi wa Sheria toka OCPD Bi. Happyphania Luena amemshukuru Kamishna kwa kutembelea banda hilo kujifunza kazi za Ofisi hiyo lakini ametambua mchango na ushirikiano walio nao kati ya OCPD na Tume hiyo ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika kuhakikisha haki na masula ya kisheria yanazingatiwa katika jamii.

“Mbele yako ni Juzuu za Sheria zilizofanyiwa Urekebu toleo la mwaka 2023 tumezileta hapa kuwaonesha wananchi na kuwalewesha kwanini toleo la mwaka 2002 limefutwa baada ya kuzindualiwa hili la mwaka 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia SUluhu Hassan lakini pia tunawapa elimu wananchi umuhimu wa kazi hii ya urekebu wa sheria zetu” alieleza Bi Happyphania.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Bwana Nyanda Shuli akioneshwa Juzuu za Toleo la Urekebu wa sheria la mwaka 2023.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Bwana Nyanda Shuli akiangalia na kufurahia kitabu cha majina ya Sheria zote za nchi zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA bwana John Pumbalu alipotembelea banda la OCPD.

Wanafunzi wakipata maelezo kuhusu mchakato wa utungwaji wa sheria kwenye banda la OCPD.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad