HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 21, 2025

SELINA, AZIZA, SHUFAA WAMO TENA UDIWANI VITI MAALUM KIBAHA MJINI

 




Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Julai 21,2025
MHARIRI wa makala gazeti la Uhuru Selina Wilson ameingia tena katika nafasi tano za madiwani viti maalum ,kupitia Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi walioshinda wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

Wengine ni Aziza Mruma aliyeongoza kwa kupata kura 952, Sara Uledi kura 864 akifuatiwa na Shufaa Mshana aliyepata kura 581 na Lydia Mgaya kura 575.

Uchaguzi huo wa ndani ya chama ulifanyika katika Ukumbi wa Nexus Kibaha na kuhusisha wagombea 15 waliowania nafasi tano za Viti Maalum kutoka Tarafa mbili ya Kibaha na Tarafa ya Kongowe.

Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo, Ally Kibwana ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mafia, alimtangaza Aziza Mruma kutoka Tarafa ya Kibaha kuwa mshindi kwa kupata kura 952 na Selina Wilson akiwa mshindi wa tano kwa kupata kura 527 kati ya kura halali 1,083 zilizopigwa.

Kwa upande wa Tarafa ya Kibaha Nafasi ya sita ni Maria Msimbe kura 420, wa saba Emiliana Sinesilya 294 ,wa nane Beatrice Manyama 192 ,tisa Rehema Abdala 103, wa kumi ni Joyce Shauri 74 na Magreth Yagaza ambaye kura zake hazikutajwa.

Upande wa Tarafa ya Kongowe,Sara Uledi, Lidya Mgaya namba tatu Mshindo aliyepata kura 343 ,nne ni Mariam Gama 180 ,wa tano Elizabeth Nyambilila 113 na Beatrice Kesi aliyejinyakulia kura 99.

Kwa mujibu wa Kibwana, Jumla ya kura zilizopaswa kupigwa zilikuwa 1,094 ambapo kura halali zilikuwa 1,083 na kura 11 ziliharibika.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT )Kibaha Mjini Eline Mgonja aliwataka washindi kuendeleza mshikamano na Umoja.

Mgonja alihimiza nidhamu na kuwaasa kuachana na makundi yasiyo na tija ili kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na madiwani mwezi Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad