Rais SAMIA SULUHU HASSAN amewapatia leseni wachimbaji wadogo wa madini na kuwafanya wachimbaji wa madini nchini kujivunia na kuweza kufanya shughuli za uchimbaji wa madini kwa kujiamini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Dhahabu Taifa (FEMATA) na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo wa madini Mkoa wa GEITA (GEREMA),TITUS KABUO amesema hayo baada ya kuhitimishwa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa GEITA zaidi ya MIA NNE iliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
Mchango wa sekta ya madini kwa pato la taifa imeongeza kutoka asilimia TISA NUKTA MOJA mwaka 2033/2024 hadi kufikia asilimia KUMI NUKTA MOJA mwaka 2024/2025 na kuchangia mfuko mkuu wa serikali Shilingi TRILIONI MOJA SUFURI SABA kwa mwaka 2024/2025.
No comments:
Post a Comment