Kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Bilioni 4.360 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya madarasa, maabara, mabweni, Bwalo la chakula Jengo la Utawala na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Njombe ambayo imekamilika.
Hayo yamebainishwa tarehe 17 Julai 2025 na Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Njombe Mwl Nelasi Mulungu ambapo amesema pia Bilioni 1.6 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Amali ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya ya Ludewa.
Mwl Mulungu amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Bilioni 12.638 kwa ajili ya ujenzi wa shule 20 za kata katika mkoa huo wa Njombe.
Pia amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika mkoa wa Njombe ikiwemo ujenzi wa Mabweni, Nyumba za walimu, na Matundu ya vyoo.





No comments:
Post a Comment