Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeshiriki zoezi la ukaguzi na majaribio ya mtambo utakaotumika kuchimba visima vitatu vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay Mkoani Mtwara.
Ukaguzi huo uliofanyikia katika Jimbo la Tianjin nchini China, ulilenga kuhakiki uimara na ufanisi wa mtambo huo kabla ya kusafirishwa kuja nchini Tanzania kwa kazi ya uchimbaji wa visima vya gesi asilia inayotarajiwa kuanza Novemba 2025.
Pamoja na ukaguzi wa mtambo huo wenye uwezo wa kuchimba hadi urefu wa mita 8000, PURA pia ilishiriki kama muangalizi katika ukaguzi na majaribio ya mifumo mbalimbali iliyopo katika mtambo huo na mabomba yatakayotumika wakati wa uchimbaji.
Hatua hii ya ukaguzi ni muhimu kwa kuwa hutoa hakikisho la ufanisi wa mtambo kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi.
PURA, kama mdhibiti wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini inashiriki na kusimamia hatua zote za mradi kuhakikisha mradi unatekelezwa kama ulivyopangwa.
Inatarajiwa kuwa, visima vitakavyochimbwa (MS-2, MB-5 na Kasa-1x), vitaongeza uzalishaji wa gesi asilia kwa zaidi ya futi za ujazo milioni 30 kwa siku.
Tuesday, July 22, 2025

Home
Unlabelled
PURA YASHIRIKI UKAGUZI NA MAJARIBIO YA MTAMBO WA KUCHIMBA VISIMA VYA GESI ASILIA
PURA YASHIRIKI UKAGUZI NA MAJARIBIO YA MTAMBO WA KUCHIMBA VISIMA VYA GESI ASILIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment