HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 14, 2025

MUHIMBILI MSHINDI WA KWANZA HUDUMA ZA AFYA SABASABA 2025.


Hospitali ya Taifa Muhimbili [Upanga & Mloganzila] imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la watoa huduma za afya katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam [Saba Saba] yaliyohitimishwa leo Julai 13, 2025.

Akizungumza katika sherehe za kufunga Maonesho hayo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezipongeza taasisi zote zilizoshiriki maonesho hayo na kuzitaka kuongeza juhudi ili kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Aidha akikabidhi Tuzo hiyo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Suleiman Jaffo ameipongeza Hospitali hiyo kwa huduma bora na za kibingwa zinazotolewa kwa wananchi.

Tuzo hiyo imetokana na ubora na utendaji kazi wa wataalam wake waliokuwa wakitoa huduma za kibingwa ambapo wananchi walipata fursa ya kupata elimu, ushauri, uchunguzi na matibabu ndani ya viwanja vya sabasaba.

Kwa upande wa wananchi waliotembelea banda la hospitali hiyo wameishukuru na kuipongeza Muhimbili kwa kuleta hospitali ndani ya maonesho na kusogeza huduma karibu yso kupitia maonesho ya sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad