HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 16, 2025

MUHIMBILI MLOGANZILA KWA MARA YA KWANZA YATOA UVIMBE KWENYE UTUMBO MPANA KWA KUTUMIA MATUNDU MADOGO.

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini imefanya huduma ya ubingwa bobezi ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo mpana kwa kutumia matundu madogo (lapascopic lower anterior resection) kwa mgonjwa aliyekuwa na changamoto hizo.

Akielezea upasuaji huo Daktari Bingwa wa Upasuaji aliyebobea kwenye Upasuaji wa Tumbo na Ini MNH-Mloganzila, Dkt. Richard Mliwa amesema upasuaji huo umechukua takribani masaa mawili, ambao ni muda mfupi ukilinganisha na upasuaji wa kufungua tumbo ambao huchukua takribani masaa manne.

Dkt. Mliwa amebainisha kuwa upasuaji huo umewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika vifaa tiba, miundombinu ya kutolea huduma na kuwajengea uwezo wataalam ambao muda wote wanatoa huduma kwa kushirikisha taaluma mbalimba hivyo kutoa matibabu stahiki kwa mgonjwa husika.

Dkt. Mliwa amefafanua baadhi ya faida za huduma hiyo ni pamoja na mgonjwa kutopata maumivu makali, mgonjwa kukaa wodini kwa muda mfupi, mgonjwa kutopoteza damu nyingi wakati wa upasuaji, mgonjwa kutokuwa na kovu kubwa na kupunguza muda wa mgonjwa kuhudumia kidonda.

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ni miongoni mwa hospitali zilizojipambanua katika kuanzisha huduma za ubingwa bobezi ambazo hazipatikani hapa nchini na kuwapunguzia usumbufu Watanzania wengi kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu hayo.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad