MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, ameisifu na kuipongeza kampeni ya Kili Challenge, ambayo ni ubia kati ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) iliyolenga kukusanya zaidi ya shs bilioni mbili za Kitanzania kwa mwaka huu, akisema inaleta nguvu mpya katika azma ya serikali ya kutokomeza UKIMWI kama janga la afya la kitaifa na kufikia malengo ya Sifuri tatu ifikapo mwaka 2030.
Aliyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki tukio la kupanda Mlima Kilimanjaro la mwaka huu, ikiwa ni mwaka wake wa 23 tangu kuanzishwa, mjini Moshi, mkoani humo mwishoni mwa wiki, akiyataja malengo hayo kuwa ni maambuki mpya sifuri, unyanyapaa sifuri na vifo dhidi ya VVU, sifuri.
“Tunapowaona vijana wakipanda mlima na kuendesha umbali mrefu kwa ajili ya kampeni hii, tunakumbushwa kuwa mapambano dhidi ya VVU ni jukumu letu sote, nawapongeza waandaaji, wadhamini na washiriki wote kwa kuonesha uongozi, ujasiri na ushirikiano wa hali ya juu.
“Hakika serikali hii ya awamu ya sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, ipo mstari wa mbele kuhakikisha jamii na watanzania kwa ujumla, wanapata huduma za VVU na UKIMWI.
“Nimesikia takwimu kuwa waliopima ni wengi lakini walioonekana kuwa na maambukizi ni wachache, hizo ni jitihada kubwa sana kwa serikali na ni jitihada kwa wananchi wanaothubutu kujitokeza kupima afya zao, kwani wapo wengi wanaoogopa zoezi la kupima.
“Nitoe wito kwa viongozi, sisi viongozi ndio tunatakiwa tuwe mstari wa mbele, tukienda katika mazoezi ya upimaji, sisi viongozi tuwe wa kwanza kupima ili wananchi wahamasike na kuiga mfano wetu kupima afya zao,” aliongeza Mhe. Babu.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja Mkuu wa GGML, Bw. Ashraf Suryaningrat, alisisitiza kuwa GGML itaendelea kushirikiana na jamii katika kuimarisha afya ya umma na uwezeshaji wa maendeleo ya jamii akisema Kili Challenge siyo tu tukio la kawaida, ni dhamira ya kiutu chini ya kaulimbiu ya mwaka huu isemayo ‘Je, ingekuaje kama tungekata tamaa?.
“Ujumbe huo umezidi kushika hatamu leo, wapandaji wetu jasiri na waendesha baiskeli wetu wamejibu wazi kuwa hawakukata tamaa kwenye kupanda mlima, hawakukata tamaa kwenye kutimiza dhamira yao, wala hawajakata tamaa kwa mamilioni ya Watanzania ambao bado wanaishi na VVU/UKIMWI.
“Ujumbe huu wa matumaini, uvumilivu, na uthabiti unaendana kikamilifu na dhamira ya Geita Gold Mining Limited (GGML) na AngloGold Ashanti hususani mwaka huu tunapoadhimisha miaka 25 ya uchimbaji wa dhahabu kwa uwajibikaji hapa Tanzania, hatuangalii tu mafanikio ya kibiashara, bali tunaenzi robo karne ya uwekezaji wa kweli katika jamii na Tanzania kwa ujumla.
“Kuanzia elimu, afya, maji safi, barabara, hadi ujasiriamali wa ndani, GGML imekuwa bega kwa bega na jamii, kauli mbiu yetu ya kimataifa ya “Uchimbaji Kuwezesha Watu na Kuendeleza Jamii” imebeba maana halisi ya uwajibikaji wa kijamii,” aliongeza kuwa mwaka huu kama sehemu ya maadhimisho hayo walifanya kitu cha kipekee kwa kupeperusha bendera ya kumbukumbu juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro, inayowakilisha miaka 25 ya ubora, uwajibikaji, ustahimilivu na ushirikiano.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne Mohamed, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela, aliwapongeza washiriki na waandaaji wa Kili Challenge kwa kujitolea kwao katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
"Kampeni hii siyo kupanda mlima tu, ni alama ya dhamira na mshikamano tunaouhitaji kama taifa katika kutokomeza VVU na UKIMWI, kwa niaba ya Mhe. Martine Shigela na Mkoa mzima wa Geita, naipongeza GGML, TACAIDS na wadau wote kwa kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika kuchangisha rasilimali na kuelimisha jamii kuhusu janga hili, jitihada zenu zinaokoa maisha na kujenga mustakabali bora kwa Watanzania wote,”Alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Samwel Sumba pamoja kupongeza ushirikiano wa pamoja uliofanya tukio hilo kuwa mfano bora wa kitaifa wa ukusanyaji wa fedha na uhamasishaji endelevu wa afya, alisema fedha zinazokusanywa kupitia Kili Challenge zinaelekezwa moja kwa moja kwa walengwa na zinatumika kwa uwazi mkubwa kusaidia huduma muhimu kote nchini Tanzania.
“Tunawashukuru washiriki wote, wafadhili wote, na hasa GGML kwa kuendelea kuwa nasi bega kwa bega, huu ni mfano wa mshikamano wa kweli katika mapambano dhidi ya VVU,” alisema.
Kampeni ya kuchangisha fedha bado inaendelea hadi Oktoba 2025, na wadau wa maendeleo, wafadhili, na umma kwa ujumla wanahimizwa kuchangia ili kuweza kufikia lengo hilo la kukusanya shs bilioni 2 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu (wa pili kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa wapanda mlima Kilimanjaro katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki kampeni ya Kili Challenge 2025 yenye dhumuni la kukusanya fedha dhidi ya mapambano ya HIV/AIDS inayoandaliwa na Geita Gold Mine kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS). Hafla hiyo ilifanyika Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Nyuma yake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne na viongozi kutoka GGML na TACAIDS.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu (wa tatu kushoto), akikabidhi cheti kwa mmoja wa wapanda mlima Kilimanjaro, katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki kampeni ya Kili Challenge 2025 yenye dhumuni la kukusanya fedha dhidi ya mapambano ya HIV/AIDS inayoandaliwa na Geia Gold Mine kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS). Hafla hiyo ilifanyika Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Nyuma yake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne na viongozi kutoka GGML na TACAIDS.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 30 kwa Mwenyekiti wa asasi ya Konga Arusha DC, Bi. Agnes Mao, ambao ni baadhi ya wanufaika wa kamapeni ya Kili Challenge katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki kampeni ya Kili Challenge 2025, yenye dhumuni la kukusanya fedha dhidi ya mapambano ya HIV/AIDS inayoandaliwa na Geia Gold Mine kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS). Hafla hiyo ilifanyika Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne na viongozi kutoka GGML na TACAIDS.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, akikabidhi mfano wa hundi ya shs 29,855,000 Mhazini wa Kikundi cha Wanawake Kilimanjaro Kupambana na Ukimwi (KIWAKKUKI), Bi. Diana Mushi, ambao ni baadhi ya wanufaika wa kamapeni ya Kili Challenge katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki kampeni ya Kili Challenge 2025 yenye dhumuni la kukusanya fedha dhidi ya mapambano ya HIV/AIDS inayoandaliwa na Geia Gold Mine kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS). Hafla hiyo ilifanyika Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne na viongozi kutoka GGML na TACAIDS.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 30 kwa Mhazini wa Kikundi cha Jali Afya yako Epuka Maambukizi Mapya Fata Ushauri Nasaha (KIJAEFA), Bw. Omari Mussa Mkhanda, ambao ni baadhi ya wanufaika wa kamapeni ya Kili Challenge katika hafla ya kuwapongeza wapanda mlima 49 na waendesha baiskeli 17 walioshiriki kampeni ya Kili Challenge 2025 yenye dhumuni la kukusanya fedha dhidi ya mapambano ya HIV/AIDS inayoandaliwa na Geia Gold Mine kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS). Hafla hiyo ilifanyika Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mhe. Sakina Jumanne na viongozi kutoka GGML na TACAIDS.
No comments:
Post a Comment