Kiwanda cha Hester Biosciences Africa Limited kilichopo katika Eneo la Viwanda la TAMCO, Kibaha – Mkoa wa Pwani, kimepokea ugeni wa wasajili wa chanjo na wakurugenzi wa uzalishaji wa chanjo za mifugo kutoka nchi 25 za Afrika terehe 18 Juni 2025.
Ziara hiyo imefanyika kama sehemu ya mkutano wa kikanda wa AU PANVAC unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 20 Juni 2025.
Kiwanda hicho, ambacho ni sehemu ya kampuni mama kutoka India – Hester Biosciences Limited – ni miongoni mwa vituo vya kisasa kabisa vya uzalishaji wa chanjo za mifugo barani Afrika. Kina uwezo wa kuzalisha dozi bilioni 1.5 kwa mwaka, kikihudumia magonjwa 27 ya mifugo kupitia aina 37 za chanjo, kwa wanyama kama kuku, ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Uwekezaji wa kiwanda hicho umegharimu Dola za Kimarekani milioni 18, sawa na takriban Shilingi bilioni 44 za Kitanzania.
Wageni waliotembelea kiwanda hicho walipata fursa ya kujionea teknolojia ya uzalishaji ikiwemo njia za Chick Embryo Origin, Tissue Culture, Fermentation, na Continuous Cell Line zinazotumika kuzalisha chanjo salama na bora kwa mifugo. Pato la kila mwaka linatarajiwa kufikia Dola milioni 30 za Kimarekani, huku ajira kati ya 150 hadi 200 zikitajwa kuendelea kutolewa pindi uzalishaji utakapo fikia kiwango cha juu.
Kwa upande mwingine, mkutano wa AU PANVAC unaofanyika katika Ukumbi wa King Jada Hotel, umeweka mkazo katika kuimarisha mfumo wa pamoja wa udhibiti, uzalishaji na usambazaji wa chanjo, hasa kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR). Huu ni ugonjwa hatari unaohatarisha ustawi wa mifugo na uchumi wa wakulima wengi barani Afrika.
Kiwanda cha Hester kimeanza rasmi uzalishaji tangu mwaka 2021 na tayari kimeshauza chanjo kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya, Zambia, Botswana, Burundi, Eritrea, Ghana, Mongolia, Nepal na Israeli. Hii inaonyesha mchango wake mkubwa si tu kwa Tanzania, bali kwa afya ya mifugo katika bara zima la Afrika.
“Ninatoa shukrani za dhati kwa uongozi na wafanyakazi wa Hester Biosciences Africa Limited kwa mapokezi mazuri na kwa kutupatia fursa ya kutembelea kiwanda hiki cha kisasa cha uzalishaji wa chanjo za mifugo. Ziara yetu leo imetuthibitishia kwa vitendo kuwa Afrika ina uwezo mkubwa wa ndani wa kuzalisha chanjo bora kwa mifugo, kwa viwango vinavyokubalika kimataifa.
Tunavutiwa sana na uwezo wa kiwanda hiki – si tu katika uzalishaji wa kiasi kikubwa cha chanjo, bali pia katika matumizi ya teknolojia ya hali ya juu, viwango vya ubora, na kujitolea kwao kuhakikisha afya ya mifugo barani. Hii ni hatua kubwa kuelekea kujitegemea kama bara katika sekta ya afya ya wanyama.

No comments:
Post a Comment