Makubaliano haya ya miaka miwili yamesainiwa tarehe 18, Juni 2025 katika makao makuu ya TADB, yakihusisha viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili.
Mkataba huo, uliosainiwa leo Juni 18, 2025 na Dkt. Mwajuma Hamza, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC na Adolphina William, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, unalenga kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo jumuishi kwa kuhakikisha wanawake na vijana wanapata fursa za kiuchumi, elimu, mikopo na msaada wa kitaalamu.
Mambo Muhimu Yatakayotekelezwa katika mkataba huo wa Miaka miwili ni pamoja na Utafiti wa Kitaifa kubaini idadi na mahitaji ya wanawake wajasiriamali kwenye sekta husika ili kuweka mikakati sahihi ya maendeleo.
Mafunzo ya kujengea uwezo kulingana na matokeo ya tafiti, ili kukuza ujuzi na utayari wa kibiashara.
Uchambuzi wa fursa za kifedha na mikopo kwa wanawake na vijana wanaojishughulisha na minyororo ya thamani ya kilimo.
Upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia huduma maalum za kifedha kutoka TADB.
Msaada wa kitaalamu (Technical Assistance) kuhusu masuala ya fedha, masoko, matumizi ya teknolojia na uzingatiaji wa viwango vya kibiashara.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Adolphina William amesema makubaliano hayo yatawawezesha wanawake na vijana kwani ndiyo njia ya kuongeza tija kwenye kilimo.
"Ushirikiano huu unathibitisha dhamira ya TADB kutoa huduma za kifedha zenye kugusa moja kwa moja walengwa wetu.”
Kwa Upande wa Dkt. Mwajuma Hamza ameeleza kuwa makubaliano haya ni hatua kubwa katika kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake katika sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment