BENDI maarufu ya muziki ya dansi barani ulaya The Ngoma Africa band yenye makao yake nchini ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki nguli Kamanda Ras Makunja inatalajiwa kutingisha jukwaa la maonyesho makubwa ya International Afrika Festival Tubingen yatakayoanza siku ya tarehe 5 hadi 8 Juni 2025 katika mji wa Tubingen uliopo kusini mwa Ujerumani ambapo Ngoma Africa band watalitingisha jukwaa siku ya jumamosi tarehe 7 Juni 2025.
Bendi hiyo yenye sifa za kuwatia wazimu washabiki wa muziki barani ulaya imejizoelea umaarufu kwa kutumia mudundo wake wa muziki wa dansi kutoka Tanzania na Afrika mashariki mrindimo ambao wameupa jina la extraordinary Rhythm "Bongo Dansi" made in Tanzania, mdundo huo wa uliofanikiwa kuwanasa washabiki barani ulaya ,umegeuka kuwa mzimu wa muziki unaotingisha majukwaa kwa takribani miaka 32 tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo mwaka 1993 na muhasisi wake mtanzania mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja.
Tamasha la International Africa Festival Tubingen,Germany ndio onyesho kubwa la kiafrika barani ulaya ambalo linatimiza kuwa onyesho la 25 mwaka huu wa 2025 ambalo linakusanya wajasiliamali,wasanii kutoka nchi mbalimbali za kiafrika ,onyesho hilo ndio gumzo la ulaya.
No comments:
Post a Comment