HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 3, 2025

TBS YATOA ELIMU YA BIDHAA ZA UBORA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZIWA MOROGORO

WATUMIAJI wa bidhaa watakiwa kusoma maelezo yanayopatikana katika vifungashio vya bidhaa kabla ya kununua bidhaa husika hususani muda wa matumizi.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Udhibiti ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Sarah Maro, wakati akizungumza na watembeleaji kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa yaliyofanyika katika viwanja vya zimoto Manispaa ya Morogoro

Alisema watumiaji wa bidhaa wanatakiwa kusoma kwa makini taarifa zilizopo kwenye vifungashio ili kuepuka kununua bidhaa zilizoisha muda wa matumizi.

"Ni muhimu wananchi wakajenga utamaduni wa kusoma taarifa hizo ili kujiridhisha kama zinakidhi matakwa ya viwango ili kuepuka gharama au hasara inayoweza kujitokeza kwa kutumia bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake," alisema Maro.

Alisema watu wanaponunua bidhaa baada ya kusoma maelezo wanakuwa na uhakika na bidhaa walizonunua hivyo kuepuka hasara ambazo zingejitokeza kwa kununua bidhaa zisizokidhi mahitaji yao hivyo kuwa salama zaidi kiuchumi pamoja na kiafya

Pamoja na hayo, Maro aliwasisitiza watumiaji wa bidhaa kutoa taarifa endapo watakutana na bidhaa zisizo na viwango au zilizoisha muda wa matumizi kwa lengo la kudhibiti bidhaa hizo kutumika.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad