HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 22, 2025

Mahindra kuja na Magari ya Umeme na Gesi Tanzania

Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey amesema Tanzania iko katika hatua za mwisho kutengeneza magari yanayotumia Umeme na Gesi nchini kupitia kiwanda cha kampuni ya GF kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari ya Mahindra Scorpio uliofanyika jijini Dar es salaam, Balozi Dey amesema kutokana na mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya serikali ya Tanzania na India,imesababisha wawekezaji wengi kutoka nchini India kuja kuwekeza nchini  Tanzania,hali inayoendeleza mahusiano mazuri yaliofanywa na Waasisi wa Mataifa hayo mawili.

"Miongoni mwa kampuni hizo ni kampuni ya magari ya Mahindra ambayo imetambulisha gari mpya katika soko la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki,lakini niseme tu kuwa magari haya kuanzia mwakani yatakuwa yakitengenezwa nchini Tanzania katika kiwanda cha GF Kilichopo Kibaha mkoani Pwani",amesema Balozi Bishwadip Dey.

Nae Mtendaji Mkuu wa kampuni ya GF Mehboob Karmali alisema ujio wa Mahindra nchini ni ukombozi, kwani leo wametambulisha Gari sokoni na baadaye watazindua gari za umeme na gesi zitakazotengenezwa nchini Tanzania kupitia kiwanda chao Kilichopo Kibaha mkoni Pwani.

"Kwa kuanza tutaanza na magari madogo 'pickup- double cabin' maalumu kwa shughuli za kilimo na wajasiliamali wadogo hasa mashambani" alisema Karmali.

Pia alizitaka tasisi za umma na serikiali kwa ujumla kujenga tabia ya kununua bidhaa kutoka kwenye  viwanda kwetu ili kuvilinda na kuongeza pato la taifa na kuokoa pesa ambayo ingetumika kuagiza bidha nje ya nchi.
 
Kampuni ya GF Automobile imezindua gari aina ya Mahindra Scorpio kwa ajili ya matumizi katika bara bara za mazingira tofauti hasa vijijini na mashambani na gesi kukabiliana na mazingira tofauti.
Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya GF Automobile, Mehboob Karmali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa gari mpya ya Mahindra Scorpio uliofanyika jijini Dar es salaam.Kulia ni  Mtendaji mkuu wa Mahindra,ukanda wa  Africa, Bobby Salwan
Balozi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari ya Mahindra scorpio
Gari aina ya Mahindra Scorpio ikitembea wakati wa uzinduzi huo

1 comment:

  1. Hii gari utatumia miaka ishirini gari ngumu Sana , mbona muandishi hakunesha gari kwa pembeni, hata land cruiser haifai mbele ya Scorpio mahindra

    ReplyDelete

Post Bottom Ad