HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 20, 2025

KAMATI YA KITAIFA YA KIZAZI CHENYE USAWA YAWAPONGEZA WANAWAKE IRINGA KWA KUTUMIA VYEMA FURSA ZA SERIKALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

 





‎ Na WMJJWM – Iringa
MWENYEKITI  wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa, Mhe. Angela Kairuki amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na wanawake wa Mkoa wa Iringa kupitia Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo tarehe 19, Juni 2025 mkoani Iringa wakati wa ziara ya kufuatilia utekelezaji wa programu hiyo katika ngazi ya mkoa pamoja na kutathmini mafanikio na changamoto katika miradi ya uzalishaji.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhe. Kairuki amesema amevutiwa na mshikamano, ubunifu na jitihada za wanawake katika kuanzisha na kuendesha miradi ya uzalishaji.

Ameongeze kuwa Kamati hiyo imefanya ziara mkoani humo kwa lengo la kutembelea miradi mbalimbali ya wajasiriamali, vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, pamoja na majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi.

‎Aidha, Mhe. Kairuki amewahimiza wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kwani fursa hizo ni nyenzo muhimu za kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
‎“Ni wakati wa kuhakikisha kuwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu mnachangamkia kikamilifu fursa zinazotolewa na serikali kuwawezesha kiuchumi” amesema Mhe. Kairuki
‎Kwa upande wake, Naibu Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa kamati hiyo, Mhe. Mgeni Hassan Juma amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usawa wa kijinsia unatekelezwa kwa vitendo katika ngazi zote za jamii.
‎Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Juliana Kibonde, amesema kuwa Wizara kupitia Idara hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha kuwa fursa mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi zinazotolewa na Serikali zinawafikia na kuwanufaisha kwa vitendo.
‎Kwa upande wa wanufaika kupitia Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa programu hiyo kwa moyo wa dhati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad