Gawio hilo limetolewa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma.
Vilevile, BRELA imepokea tuzo kama Taasisi iliyofanya vizuri katika kuchangia gawio kila mwaka, kwa wastani wa Shilingi Bilioni 16.8 kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi husika, wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya BRELA, Prof. Neema Mori, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa.




No comments:
Post a Comment