Hayo yameelezwa leo Juni 17, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati Kampuni hiyo ikiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Suleiman Serera
Naibu Katibu Mkuu amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi nchini ikiwemo kampuni hiyo katika kukuza uchumi wa Taifa, kuhimiza ajira, na kuendeleza mazingira bora ya biashara nchini.
“Dira yetu ya ukuaji endelevu inategemea ushiriki wa sekta binafsi kwa kiwango kikubwa. Tunazihimiza biashara za ndani kuangalia nje ya mipaka ya taifa na kuchangia kuiweka Tanzania katika nafasi ya ushindani wa kiuchumi kupitia viwanda,” amesema.
Kwa upande wake Mkuurgenzi Mtendaji wa SSB, Ali Mukadam amesema wameongeza uwezo wa uzalishaji wa unga wa ngano kwa kiasi kikubwa kutoka tani 15 kwa siku ilipoanzishwa hadi tani 9,000 kwa siku katika shughuli zake kote barani Afrika.
Amesema katika maadhimisho hayo pia wamezindua chapa mpya ya Miaka 50 ya Bakhresa Group na cha chapa mpya ya Kifurushi cha unga wa ngano unaozalishwa na kampuni hiyo.















No comments:
Post a Comment