HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 14, 2025

WANACHAMA TEN/MET WACHANGIA MILIONI 35 KUBORESHA ELIMU HALMASHAURI YA MPIMBWE

 

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro akizungumza na wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi, halmashauri ya Mpimbwe.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro akizungumza na wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi, halmashauri ya Mpimbwe.

Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza na wadau wa elimu kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi, halmashauri ya Mpimbwe.

Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akisisitiza jambo kwenye kwenye hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi, halmashauri ya Mpimbwe.

Mgeni Rasmi, katika hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela (wa pili kulia) kikabidhi zawadi kwa walimu waliofanya vizuri katika ufundishaji kwenye shule zao, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yanafanyika kitaifa mkoani Katavi, Halmashauri ya Mpimbwe. Wa kwanza kulia  ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania, Bw. Simon Nanyaro.

Mgeni Rasmi, katika hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa (GAWE) 2025, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela (wa pili kulia) kikabidhi zawadi kwa walimu waliofanya vizuri katika ufundishaji kwenye shule zao, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yanafanyika kitaifa mkoani Katavi, Halmashauri ya Mpimbwe. Wa kwanza kulia  ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania, Bw. Simon Nanyaro.

Na Mwandishi Wetu, Katavi

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwa kushirikiana na wanachama wake, imekusanya nguvu ya pamoja na kujitolea kiasi cha shilingi milioni 35,000,000 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Halmashauri ya Mpimbwe, mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliofanyika mkoani hapa.

Akizungumza katika hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi, halmashauri ya Mpimbwe, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania, Bw. Simon Nanyaro alisema wametoa fedha hiyo ili iweze kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu katika Mkoa wa Katavi.

Akifafanua zaidi Bw. Nanyaro alisema wameguswa na muitikio mkubwa wa wazazi/walezi, viongozi wa mila na dini katika shule walizozitembelea wakiwa katika ziara za maadhimisho kwani walijumuika pamoja kujadili mambo mbali mbali muhimu yanayohusu elimu, ikiwemo jitihada kubwa za walimu katika kuendelea kuwafundisha wanafunzi wengi licha ya changamoto zinazowakumba katika mazingira ya ufudishaji hali inayoonyesha kufanya kazi kwa bidii, kujitolea na dhamira ya kuinua kiwango cha Elimu nchini.

"Tumeshuhudia changamoto kadha wa kadha zinazozikabili shule zetu zinazohitaji kushughulikiwa ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji: ikiwemo upungufu na uchakavu wa miundombinu ya madarasa kwa baadhi ya shule, upungufu wa walimu, hasa wa kike, ukosefu nyumba za walimu, hasa katika baadhi ya shule, ukosefu wa mabweni kwa wanafunzi, hasa wanaotoka vijiji vya mbali, unaolazimu watoto kutembea hadi kilometa 12 kila siku Kwenda na kurudi shuleni jambo linalochangia utoro na wengine kuacha shule kabisa." Alisema Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Bw. Nanyaro.

Aidha wadau hao wa elimu walipendekeza msaada walioutoa kusaidia kutatua changamoto ya jumla ya madawati 407 meza 10 na viti 10 kwa mchanganuo ufuatao; Madawati 250 yaende shule ya Msingi Migunga, Madawati 47 yasaidie Shule ya Msingi Ikulwe, Madawati 110 yapelekwe katika Shule ya Msingi Minyoso na meza 10 na Viti 10 ziende kwa ajili ya walimu wa shule ya sekondari Mirumba.

Pamoja na hayo walipendekeza viongozi wa Serikali kuandaa mpango na kutenga bajeti ya ujenzi wa hostel za wanafunzi wa kike na wakiume, kujenga matundu ya vyoo, vyumba vya kujisitiri wanafuzi wa kike wakati wa hedhi na upatikanaji wa maji safi na salama; utakaoendana sambasamba na ujenzi wa madarasa ili kukidhi uhitaji uliopo kwa sasa ili kulinda afya na usalama wa Watoto.

Wada wa elimu tunashauri viongozi katika sekta ya elimu ngazi ya wilaya na mkoa kuandaa ziara za mara kwa mara kutembelea shuleni kukutana na wanafunzi, walimu, kamati za shule na wazazi/walezi kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wanafunzi na walimu shuleni.  

"...Tunawahimiza wazazi na walezi kuendelea kuchangia utoaji wa chakula na lishe shuleni ili wanafunzi wapate chakula wakiwa shuleni na kusoma bila njaa ili kuongeza ufaulu wao na kupunguza utoro shuleni. Kuzingatia sheria na Kanuni za utoaji wa adhabu kwa Wanfunzi kama ilivoelekezwa kwenye Waraka wa Elimu No. 24 wa mwaka 2002, unaotoa mwongozo namna ya utolewaji wa adhabu ya viboko shuleni. ili kuepuka kutoa adhabu kali za viboko kwa wanafunzi shuleni," alisema Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Bw. Nanyaro akiwasilisha taarifa ya wadau wa elimu baada ya kilele cha maadhimisho.

Baadhi ya viongozi na wananchi wakiwa katika hafla ya  Maadhimisho ya kilele cha Juma la Elimu (GAWE) 2025, katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakijisomea vitabu mbalimbali ndani ya Banda la Room to Read Tanzania kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, katika Halmashauri ya Mpimbwe.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakijisomea vitabu mbalimbali ndani ya Banda la Room to Read Tanzania kwenye kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) 2025, katika Halmashauri ya Mpimbwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad