HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 14, 2025

TUTAKWENDA KUWA CHACHU YA UONGOZI - MKURUGENZI TACAIDS

 


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
WAHITIMU wa mafunzo kutoka Taasisi za Umma na wametakiwa kwenda kuwa mabalozi wazuri na kuleta mabadiliko katika sehemu wanazoziongoza sambamba na kuwathamini wananchi wa hali ya chini.

"Elimu hii mliyoipata katika mafunzo yenu ya siku tano mkaifikishe mbali , binafsi nimevutiwa sana na mbinu za mafunzo haya ambapo Uongozi wa Shule unatumia wa kuwatumia wataalamu wabobezi kwenye masuala mbalimbali ,wakiwamo wastaafu kwenye kada zote hapa nchini hili ni jambo jema" amesema mgeni rasmi wakati akifunga mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Mhe. Xavier Daudi .

"Mnapaswa kufahamu na kutii miiko ya uongozi kwa sababu unapokuwa unaongoza tambua kuwa wewe ni kioo cha jamii" amesema Mhe. Xavier.

Amesema kuwa wahitimu hao ambao wameshiriki katika mafunzo yao ya (Sustainable Leadership & Magement of Public Sector Enterprises SLM -PESA Training Program ) washiriki hao wametoka katika taasisi na mashirika wanapaswa kutambua kuwa wao ni wenye bahati kwani hata wenzao huko walikotoka wanatamani wangepata fursa hiyo hivyo waende kugawana ujuzi katika maeneo yao pindi watakaporudi kwenye sehemu wanakoongoza.

"Elimu mliyoipata hapa ya usalama wa taifa, majumui, utawala bora uwajibikaji na uadilifu ni yenye tija huku tukiamini kwamba tumepanda mbegu nzuri kwa viongozi waminifu na waadilifu" amesema Xavier.

Aidha amewaasa wahitimu hao kuzingatia kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia ikiwamo kujifunza zaidi kuhusu akili unde ambayo hivi sasa inakua kwa kasi lakini kamwe wasikubali kuongozwa nayo jiwekeni tauari kukabiliana na na mabadiliko ya teknolojia" amesema.

"Mafunzo haya yamekuja kwa wakati sahihi kwani viongozi wazuri huandaliwa hivyo tunatarajia mtakwenda kutumia elimu mliyoipata hapa kuleta mabadiliko na kuwandaa viongozi wajao kuanzia katika ngazi za kazi zenu" amesema.

Mwisho amewasisitiza wahitimu hao 40 kuwa hivi sasa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu wakawahimize wanaowaongoza kujiandikisha na kujihakiki kwenye daftari la mpiga kura la kudumu na siku ya kupiga kura itakapofika kila mmoja akapige kura kwani hiyo ni haki ya kila mtanzania kikatiba.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS Dkt. Catherine Joachim ametoa shukrani kwa uongozi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwajengea uwezo na kusisitiza utaratibu huu uwe endelevu .

"Mafunzo tuliyoyapata yamegusa uongozi wa kikanda na bara la Afrika kwa ujumla na kutujengea dhana ya kuwa kiongozi bora ni poamoja na kutumikia wale unaowaongoza kwa moyo mmoja" amesema Dkt. Catherine.

Amesema kuwa "tunaahidi kuwa tunakwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika taasisi zetu " amesema Dkt. Catherine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad