UJUMBE kutoka Benki ya Dunia (WB) ukiongozwa na Claudia Zambra umeoneshwa kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Zanzibar.-
Wakizungumza baada ya kutembelea mradi wa miti katika eneo la Bungi Mkoa wa Kusini Unguja ambao uliibuliwa na wanufaika wa mfuko huo, wajumbe hao wamesema wataendelea kuisadia Serikali katika mipango yake na kuboresha vipato vya wananchi.
Akizungumza katika eneo hilo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Salhina Mwita Ameir amesema ujumbe huo kutoka WB wakiwa ni miongoni mwa wadau wanaosaidia kutoa fedha za TASAF, umekuja kujionea namna miradi inayotekelezwa inavyosaidia jamii.
“Lengo hasa ni kuja kujionea miradi inayotekelezwa na wamesema hapa namna alivyoridhika na jinsi miradi inavyosaidia wananchi masikini na kuendeleza vipato vyao,” amesema
Amesema katika ziara hiyo wamejionea wenyewe shamba la miti ambalo limeibuliwa na wanajami kama mradi mdogo kwa ajili ya kutunza mazingira na kama kisomo kwa wanajamii wengine watekeleze kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake, Meneja wa Miradi ya Ajira ya muda na uendelezaji wa miundombinu TASAF, Paul Kijazi amesema Wajumbe hao wamepongeza hatua iliyofikiwa na Tanzania na miradi imeonekana dhahiri namna inavyoleta tija na wananchi wenyewe na kuchangia kiasi kikubwa katika utunzaji na uendelezaji wa mazingira na kudhibiti athari hasi za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema kwasasa TASAF wapo katika hatau za kuandaa mradi awamu ya tatu na tayari wamefika katika hatua ambayo tathmini kama hizo zinachangia katika kuboresha miradi mingine.
“Kwakuwa tunatarajia kuanza awamu nyingine basi tathmini kama hizi ni muhimu kufanyika kwahiyo hata hawa benki ya dunia wapo kwenye ukaguzi ili kutekeleza miradi mingine katika awamu zinzofuata,” amesema.
Amesema katika awamu inayotarajiwa kuanza katika upnde wa ustawishaji wa jamii na kuongeza kipato watajikita zaiid katika miradi ya mabadiliko ya tabianchi ikizingatiwa nchi inavyokabiliwa na tatizo hilo.
Nao baadhi ya wanufaika wa TASAF, Dawa Haji Ali wa shehia ya Bungi amesema awali alikuwa akiishi maisha magumu lakini baada ya kuanza kupokea Tasaf alinunua taitai na kamba kwa ajili ya kulima mwani akaanza kusomesha watoto wake na ansshukuru wamemaliza shule.
Amesema kupitia Tasaf amenunua mbuzi na amejenga nyumba na maisha yake yapo vizuri.Wakati Suleiman Haji amesema kabla ya Tasaf maisha yake yalikuwa magumu sana lakini baada ya kumuwezesha akaanza kununua boti ya Sh200,000 kuingia baharini kuvua.
“Bahati siku zikienda nikawa napata mafao nanunua vitu vingine na baadaye nikanunua ngalawa kubwa ambayo sahivi ninakwenda na wenzagu maji mengi na tunapata mafao,” amesema
Amesema kwasasa yupo kwenye ujenzi, anasomesha watoto wake mmoja yupo sekondari na anamlipia mahitaji yake yote bila changamoto.
Mnufaika mwingine Ashura Mzee Matabi amesema ameingia Tasaf miaka 10 iliyopita mwanzo alikuwa hana nyumba, lakini amepta kiasi akajenga nyumba.


No comments:
Post a Comment