HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 10, 2025

CCM Kata Msasani wampa ‘mitano’ mengine Rais Samia, wafanya ziara Morogoro kwa SGR

 



Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Wajumbe wa Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Msasani wamefurahishwa na utelekelezwaji wa ilani ya chama hicho na kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini na kumchagua tena Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuingoza nchi kwa miaka mitano ijayo.

Hayo yalisemwa na wajumbe hao walipokuwa wakifanya ziara maalum mkoani Morogoro kwa kutumia usafiri wa Treni ya mwendokasi (SGR) kutoka Jijini Dar es Salaam.

Safari hiyo iliyoandaliwa na na Diwani wa Kata ya Msasani Bw. Luca Neghest imewajumuisha wajumbe na wanachama wa CCM zaidi ya 40.

Akizungumza kabla ya kusafiri, Bw Neghest alisema kuwa wameamua kufanya ziara hiyo maalum mkoani Morogoro ikiwa ni kuhamasisha Watanzania kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa amani na kumchagua Dkt Samia kuwa Rais na Dkt Emmanuel John Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza kuwa Makamu wa Rais.

“Tumeamua kusafiri kwenda Morogoro kwa njiaya SGR ambayo ni matunda ya uongozi bora wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, safari yetu ni ishara ya umoja uliotukuka wa Kata ya Msasani.

Pia safari hii ni kusheherekea jinsi gani Rais Samia Suluhu Hassan anavyotekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM na Watanzania wanafurahia maendeleo katika sekta mbalimbali.

Hii safari pia ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani kwani Morogoro kuna vivutio mbalimbali vya utalii,” alisema Bw Neghest ambaye ndiye aliyegharamia Safari nzima.

Amesema utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM umefanikiwa kwa ushirikiano mkubwa wa wana Msasani kwa pamoja hivyo wanapaswa kupongezwa.

kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msasani, Bw Nyerere Mnyupe alisema kuwa Kata ya Msasani inaunga mkono juhudi za dhati za serikali ya Rais Samia kuleta maendeleo chanya kwa Watanzania na kudumisha amani.

Bw Mnyupe alisema kuwa wana-Msasani wapo bega kwa bega na Rais Mama Samia na diwani wao, Bw Neghest ambaye ameweza kuleta maendeleo katika kata yao na wananchi wanaishi kwa kushirikiana.

“Kwa kifupi, hakuna mtu ambaye hatambui kazi kubwa ya kuleta maendeleo hapa nchini inayofanywa na Rais Samia na serikali ya CCM. Tumefarijika sana na utendaji wake na uchaguzi huo ni lazima ashinde na kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo,” alisema Bw Mnyupe.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa Makangira wa Kata ya Msasani, Bi Daima Issa alimpongeza Rais Samia kwa uongozi bora wa kuiendeleza na kuifungua nchi kwa kuleta maendeleo chanya na kuwaomba wanawake wote kutosita kumchagua tena kwa miaka mitano.

“Hii safari ni ishara ya ushirikiano wa kata ya Msasani na jinsi gani Diwani Bw Neghest anavyo himiza umoja na ushirikiano. Wana Msasani tupo kitu kimoja na ndiyo maana tunasafiri kwa njia ya SGR, haya ni matunda ya uongozi bora wa Mama Samia,” alisema Bi Daima.

Diwani wa  Kata ya Msasani Bw. Luca Neghest akizungumza kabla ya kuwangoza wanachama wa CCM zaidi ya 40 kusafiri Morogoro kwa njia ya Treni ya Mwendokasi ya SGR. Ziara hiyo ni sehemu ya kudumisha umoja wa wana-CCM wa Kata ya Msasani, kutekeleza Ilani ya CCM na kufanya utalii wa ndani wenye lengo la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa Oktoba.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msasani, Bw Nyerere Mnyupe akizungumza kabla ya kusafiri kwenda Morogoro kwa treni ya SGR. Ziara hiyo imeandaliwa na Diwani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghest ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora.
Mwenyekiti wa CCM wa Makangira katika Kata ya Msasani, Bi Daima Issa akizungumza kabla ya kusafiri kwenda Morogoro kwa treni ya SGR. Ziara hiyo imeandaliwa na Diwani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghest ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora.
Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Msasani wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Stesheni ya SGR kabla ya safari ya Morogoro a iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghest ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora 

Wajumbe wakiwa ndani ya Stesheni ya mwendokasi ya SGR tayari kwenda Morogoro kufuatia ziara iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghest ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora.

Wajumbe wakiwa ndani ya Stesheni ya mwendokasi ya SGR tayari kwenda Morogoro kufuatia ziara iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Msasani, Bw Luca Neghest ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa uongozi bora.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad