HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 8, 2025

TRA KUWAPATIA MILIONI 200 WABUNIFU NA WATOA TAARIFA YA WAKWEPA KODI

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumza wakati wa kufungua kongamano la kwanza la kodi lililoandaliwa na Chuo cha Kodi (ITA) leo Mei 8, 2025, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo, akizungumza wakati wa kufungua kongamano la kwanza la kodi lililoandaliwa na Chuo cha Kodi (ITA).  leo Mei 8, 2025, jijini  Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo Naibu Waziri wa Nchi,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la kodi lililoandaliwa na Chuo cha Kodi (ITA).  leo Mei 8, 2025, jijini  Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo, akigonga kengele kuashiria uzinduzi rasmi wa tuzo mbili  ya mtoa taarifa za Wakwepa Kodi na ya Wazo Bunifu la Kusaidia Watu Kulipa Kodi kwa Hiari. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2025, jijini Dar es Salaam. Pembeni yake amayepiga makofi ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Yusuph Mwenda Uzinduzi huo umefanyika wakati akifungua Kongamano la Kwanza la Kodi lililoandaliwa na Chuo cha Kodi (ITA).



SERIKALI imetoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ukwepaji wa kodi kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),huku ikizindua rasmi tuzo mbili mpya kwa mtoa taarifa na mtoa mawazo bunifu.

Wito huo umetolewa leo Mei 8, 2025 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo wakati akifungua Kongamano la Kwanza la Kodi lililoandaliwa na Chuo cha Kodi (ITA) na kuwakutanisha  wadau mbalimbali wa sekta ya kodi na biashara.

Nyongo amesema serikali kwa kushirikiana na TRA, imeanzisha tuzo maalum ya kuwatambua na kuwazawadia wananchi wanaotoa taarifa za kweli kuhusu watu au kampuni zinazokwepa kodi.

“Ukitoa taarifa ya mtu anayekwepa kodi na ikathibitika kuwa sahihi, utazawadiwa kati ya shilingi milioni moja hadi milioni 20. Hii ni fursa ya wananchi kushiriki kulinda uchumi wa nchi hivyo TRA itatoa namba maalum ya wazi itakayowezesha wananchi kutoa taarifa hizo kwa njia salama na kwa usiri mkubwa.
,” amesema Nyongo.

Mbali na tuzo hiyo, TRA pia inazindua tuzo ya ubunifu ambayo inalenga kutambua na kuhamasisha wananchi, hususan vijana, kuwasilisha mawazo yatakayosaidia kuongeza ukusanyaji wa kodi kwa njia rahisi na rafiki.

“Kama una wazo ambalo linaweza kusaidia serikali kupata kodi zaidi, lete TRA. Tukilitumia, tutakupa zawadi. Vijana waliomaliza vyuo wasikae kimya  kwani hii ni fursa ya kuonyesha uzalendo wa nchi yetu kwa vitendo,” amesisitiza.

Aidha ,Nyongo amekipongeza Chuo cha Kodi kwa kuandaa jukwaa hilo la kitaalamu,kwani linaweka msingi wa majadiliano ya wazi kati ya serikali na walipa kodi,na kujenga mazingira rafiki ya ulipaji kodi bila shuruti.

"Lengo si kumlazimisha mtu alipe kodi, bali ni kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kwa hiari na kwa kufuata sheria. Kodi isiogopewe kodi ni fahari ya mzalendo,” amesema.

Naye, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesema kongamano hilo ni nafasi muhimu ya kupata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwa wadau, kutambua ni maeneo yapi yanahitaji kuboreshwa, na kuongeza ufanisi wa Mamlaka katika kusimamia mapato ya serikali.

 “Ni kupitia majukwaa haya ndipo tunajua wapi tumekosea, wapi tunafanya vizuri, na nini kifanyike ili kuongeza wigo wa walipa kodi huku tukikuza biashara,” amesema Mwenda.

Kwa upande wake,Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo amesema kongamano hilo limekusudia kujadili changamoto na kutoa majibu ya pamoja kwa suala la ulipaji kodi nchini.

"Tunahitaji kujua kwa nini baadhi ya watu hawalipi kodi au hawalipi kodi sahihi. Kupitia majadiliano haya tutapanua uelewa na kushirikiana kusaidia serikali kupata kodi stahiki,” amesema Profesa Jairo.

Kongamano hilo linafanyika kwa mara ya kwanza na linatarajiwa kuwa jukwaa la kudumu la mijadala kuhusu masuala ya kodi, likilenga kuimarisha uhusiano kati ya walipa kodi na mamlaka za serikali.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad