Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Mwajuma Lingwanda akimkabidhi fulana ya NACTVET Rais wa TAHLISO Geofrey Kiliba yenye ujumbe wa kampeni ya "Mwanachuo Smart'' iliyofanyika katika ofisi za NACTVET Kanda ya Mashariki ya kuwajengea uelewa wanafunzi wa vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET juu ya mifumo ya kidigitali ya kuwarahisishia huduma mbalimbali popote walipo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Mwajuma Lingwanda akimkabidhi chapisho la NACTVET Rais wa TAHLISO Geofrey Kiliba mara baada ya kuzinduliwa kampeni ya "Mwanachuo Smart'' iliyofanyika katika ofisi za NACTVET Kanda ya Mashariki ya kuwajengea uelewa wanafunzi wa vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET juu ya mifumo ya kidigitali ya kuwarahisishia huduma mbalimbali popote walipo.
Baadhi ya wanafunzi mbalimbali walioshiriki Kampeni ya uzinduzi wa Mwanachuo Smart ya NACTVET.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt.Mwajuma Lingwanda akizungumza katika Uzinduzi wa kampeni ya "Mwanachuo Smart'' iliyofanyika katika ofisi za NACTVET Kanda ya Mashariki ya kuwajengea uelewa wanafunzi wa vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET juu ya mifumo ya kidigitali ya kuwarahisishia huduma mbalimbali popote walipo.

*Dkt.Mwajuma aweka mpango mkakati kutoa huduma bora wanafunzi
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limezindua Kampeni ya Mwanachuo Smart inayomuwezesha mwanafunzi kupata taarifa za Kidijitali katika Chuo anachosoma.
Kampeni hiyo imekuja kutokana na wanafunzi kufunga safari kwa ajili ya changamoto zinazowakabili katika vyuo wanavyosoma ni pamoja kujua program wanazosoma zimesajiliwa.
Akizungumza wakati uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika Ofisi za NACTVET Kanda ya Mashariki Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Mwajuma Lingwanda amesema program hiyo inakwenda kutatua tatizo la wanafunzi kutokana na taarifa zote ziko kidijitali watazipata katika "Mwanachuo Smart".
Kampeni hiyo imezinduliwa imezinduliwa kwa kuhudhuriwa na viongozi wa TAHLISO pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
Dkt.Mwajuma amesema Kampeni ya "Mwanachuo Smart'' inalenga kuwajengea uelewa wanafunzi wa vyuo vinavyosimamiwa na NACTVET juu ya ajili ya kuwarahisishia huduma mbalimbali popote walipo.
Amesema wanafunzi walikuwa wanapata changamoto za kusafiri hadi katika ofisi za Baraza ambapo sasa hawataweza kusafiri umbali mrefu.
Hata hivyo amesema Kampeni ya "Mwanachuo Smart" watafundishwa wanafunzi wauelewe ili kuleta matokeo chanya kwao katika kuutumia mfumo huo.
Rais wa TAHLISO, Geofrey Kiliba amesema mfumo wa Kidijitali unakwenda kutatua changamoto za wanafunzi vyuo walizokuwa wanakutana nazo.
Kiliba amesema kuwa amesema kuwa walifanya ziara za kutembelea vyuo kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo ambapo NACTVET imetoa suluhisho kwa wanafunzi wa vyuo vya kati.
Amesema kuwa wanafunzi kwa sasa itaondoa changamoto kusoma program ambazo hazijasajiliwa kutokana mfumo huo inaonyesha program husika zilizosajiliwa.
No comments:
Post a Comment