Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (katikati) akikata utape ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo kwa Vitendo, Tiba za dharura na Ajali katika Kampasi ya Mloganzila.
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amezindua rasmi ujenzi wa hospitali ya kisasa ya magonjwa ya moyo na mishipa ya damu itakayohudumia wagonjwa kutoka Tanzania, Afrika Mashariki na nchi nyingine.
Hospitali hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupitia Kituo cha Umahiri cha Sayansi ya Moyo Afrika Mashariki kilichopo Mloganzila, Dar es Salaam. Mradi huu umefadhiliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Katika uzinduzi huo uliofanyika Mei 23, 2025, Profesa Mkenda pia alizindua Maabara ya Dharura kwa Mafunzo kwa Vitendo (Tanzania Emergency Care Simulation Centre Coordination Hub), kituo cha kimkakati kwa mafunzo ya hali halisi kwa wahudumu wa afya kwenye huduma za dharura. Vilevile, alizindua magari mawili ya wagonjwa.
Akizungumza katika tukio hilo, Profesa Mkenda alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia kupambana na ugonjwa wa moyo unaosababisha vifo milioni 17.9 duniani, na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi, utalii tiba, na kuongeza idadi ya wataalamu wa moyo nchini.
“Uwepo wa kituo hiki umewezesha kuanzishwa kwa programu mpya tano za shahada ya uzamili na stashahada zinazohusiana na magonjwa ya moyo, pamoja na tafiti zitakazosaidia kubaini ukubwa na vyanzo vya magonjwa hayo,” alisema Profesa Mkenda
Aliongeza kuwa awamu ya kwanza ya mradi ilihusisha ujenzi wa maabara, kumbi za kufundishia na ukumbi wa mazoezi kwa ajili ya kufundishia wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
“Hospitali hii ya kwanza ya aina yake Afrika Mashariki, itatoa huduma za kibingwa pamoja na kuwa kituo cha mafunzo na tafiti. Pia, itaiunga mkono Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika kutoa huduma bora zaidi,” aliongeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo hicho, Dkt. Rodrick Kisenge, alisema changamoto za ugonjwa wa moyo zinaweza kupunguzwa kwa kuwa na wataalamu wa kutosha na miundombinu madhubuti. Alisema kwa mujibu wa WHO, magonjwa ya moyo husababisha asilimia 32 ya vifo duniani huku asilimia 37 ya vifo hivyo vikitokea kabla ya muda hasa katika nchi za kipato cha chini na kati.
“Kuna uhaba mkubwa wa wataalamu wa moyo Afrika – kwa mfano, daktari mmoja wa upasuaji wa moyo kwa kila watu milioni 25, ikilinganishwa na kiwango cha dunia cha daktari mmoja kwa watu milioni moja. Hali hii husababisha watoto wengi kukosa huduma ya upasuaji kwa wakati,” alisema Dkt. Kisenge.
Alieleza kuwa kituo hicho kilipatiwa dola za Marekani milioni 10.2, lakini fedha hizo hazikutosha, hivyo mchakato wa awamu ya pili unaendelea ili kupata fedha zaidi kwa utekelezaji kamili wa majukumu ya kituo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa, alisema kituo hicho kitakuwa chanzo cha ajira, mabadilishano ya wataalamu, na kukuza utalii wa tiba ndani ya Afrika Mashariki.
“Serikali imewekeza vya kutosha katika sekta ya afya kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa na kuboresha huduma. Kituo hiki kitachangia sana kuongeza wataalamu wa moyo na mishipa ya damu,” alisema Profesa Kamuhabwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha MUHAS, Marsha Macatta Yambi akizungumza na waandishi wa habari wakati uzinduzi wa mradi wa awamu ya pili wa ujenzi na uendelezaji wa Kituo cha Umahiri wa Sayansi ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa na MUHAS.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (katikati) akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi mradi wa awamu ya pili wa ujenzi na uendelezaji wa Kituo cha Umahiri wa Sayansi ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) katika hafla iliyofanyika Mei 23, 2025, jijini Dar es Salaam katika
Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa awamu ya pili wa ujenzi na uendelezaji wa Kituo cha Umahiri wa Sayansi ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua mradi wa awamu ya pili wa ujenzi na uendelezaji wa Kituo cha Umahiri wa Sayansi ya Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

No comments:
Post a Comment