Mwamvua Mwinyi, Rufiji Mei 6,2025
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Mary Chatanda, amepokea mradi mkubwa wa vifaa vya ujasiriamali wa upishi na gari jipya kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa UWT Mkoa wa Pwani kutoka kwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa, Hajat Mariam Ulega.
Mradi huo ambao umetolewa na Mbaraza huyo mei 6,2025 ambapo umejumuisha gari aina ya Alphard (G) lenye namba za usajili T 912 ELT, pamoja na vifaa vya kisasa vya upishi ikiwemo sahani za udongo 200 ,vikombe vya chai 200 ,bakuli za supu 200,Glass za udongo 200 na saving dish 10.
Pia Mama Ulega alitoa majiko mawili ya gesi ya kisasa,sufuria kubwa 12,madeli 2,chupa za chai 4,miko 8,Mbakuli mikubwa ya udongo 10 na matray 4 ya kubebea vyombo
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, katika ziara yake aliyoianza mkoani Pwani, Chatanda aliipongeza UWT Mkoani humo kwa kazi kubwa na ubunifu katika kuimarisha jumuiya.
Alisisitiza kuwa ,mradi huo wa kiuchumi utaongeza tija na kuimarisha miradi ya maendeleo inayowahusisha wanawake katika mkoa huo.
Aidha, Chatanda alihimiza mshikamano na kuwataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao, wakihakikisha ushindi mkubwa kwa chama na kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Umoja wetu ndio msingi wa ushindi wetu, Tuimarishe mshikamano wetu na tuhakikishe Dkt. Samia anapata kura za kishindo, kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa," alisema Chatanda.
Awali akikabidhi vifaa hivyo Mariam Ulega alieleza , kutoa ni mazoea moyo kila mtu anao.
Alifafanua , gari hiyo itasaidia kuzisaka kura za Rais Dk Samia na ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Mapokezi ya Chatanda huko Rufiji yalipambwa na hamasa kubwa kutoka kwa wananchi na viongozi wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa UWT Mkoa, Zainabu Matitu Vulu, Mkuu wa Mkoa Abubakary Kunenge, Waziri wa TAMISEMI na MNEC wa Mkoa Mohamed Mchengerwa, Wabunge wa Viti Maalum pamoja na viongozi wa kisiasa na serikali kutoka mkoa wa Pwani.

No comments:
Post a Comment