HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 1, 2025

KATA YA MABOGINI YAPOKEA ZAIDI YA BILIONI 1.8 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA.


NA WILLIUM PAUL, MOSHI

KATA ya Mabogini imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. 

Hospitali hii ni ya wakazi wa Halmashauri ya Moshi ambayo imejengwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kuzisogeza karibu na wananchi. 

Hospitali hiyo ambayo bado haijakamilika, imeshaanza kutoa huduma ambapo Majengo yaliyokamilika ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, Jengo la Mama na Mtoto, Jengo la Kufulia, Stoo ya Madawa na Jengo la Utawala.

Hospitali hii itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa maeneo ya tambarare inayobeba Kata za Mabogini, Arusha Chini, Maeneo ya Tambarare ya Kata za Oldmoshi Magharibi,  na Kimochi, Kahe Magharibi na Kahe Mashariki.

Hospitali hii imepatikana kwa juhudi za Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini  Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Mabogini  Dkt. Bibiana Massawe. 




 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad