Inadaiwa kwamba, siku hiyo Ramadhan Samson, Operator (dereva wa mtambo) akiwa kazini na mtambo huo alibainika kuiba mafuta kutoka kwenye tenki la mtambo huo kwa kushirikiana na watuhumiwa wengine na kati yao wawili wamekamatwa (majina yanahifadhiwa); baada ya walinzi kubaini tukio hilo walianza kufuatilia ili wawakamate.
Ramadhani Samson alipogundua walinzi wanaelekea ilipo mashine, alikurupuka na kukimbia huku akiacha mtambo huo uliokuwa umewashwa ukajiongoza wenyewe na kwenda kugonga nyumba hizo na kuwajeruhi watu hao waliokuwa ndani kisha mtambo huo kukwama kwenye majaruba.
Uchunguzi wa tukio hili unaendelea kufanyika sambamba na kumtafuta operator kwa ajili ya hatua za kisheria.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Geita
Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa tukio la ajali iliyohusisha Bulldozer lenye Na. BGC-BD-002 mali ya Mgodi wa Backreef uliopo wilayani Geita kusababisha majeruhi kwa watu wanne na uharibifu wa nyumba tatu na nguzo ya moja ya umeme. Tukio hili limetokea April 02, 2025 saa 2 usiku katika Kitongoji cha Isangilo, Kata ya Lwamgasa wilaya ya Geita.Waliojeruhiwa ni Pauline Charles (35) na mtoto Majaliwa Charles (umri wiki mbili) wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Geita. Wengine ni Philipo Ngh’abi (14) na Mussa Michael (09) walipata michubuko walitibiwa na kuruhusiwa.
No comments:
Post a Comment