HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 14, 2024

Serikali Kuendelea na Uwekezaji Katika Teknolojia ya Matibabu

 


Waziri wa Afya Jenister Muhagama (katikati),Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi  Shirikishi  Muhimbili (MUHAS), Apolinary Kamuhabwa (kulia) na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotte Ozaki Macia ( kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi  wa jukwaa la nne la  Afya ya Kidijitali na Ubunifu Tanzania linalofanyika katika chuo cha Muhas tawi la Mloganzila jijini Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Apolinary Kamuhabwa (kushoto) akimkabidhi  waziri Jenister Muhagama zawadi ya kumshukuru kwa kufungua Jukwaa la 4 la Afya ya Kidijitali na Ubunifu Tanzania linalofanyika katika chuo hicho Tawi la Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Jenister Muhagama akizunguma na waandishi wa habari baada ya ufunguzi Jukwaa la nne la Afya ya Kidijitali na Ubunifu Tanzania linalofanyika katika chuo hicho Tawi la Mloganzila jijini Dar es Salaam  kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Apolinary Kamuhabwa.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuboresha Teknolojia ya Kidigitali katika sekta ya afya ili kuhakikisha usanifu zaidi kwenye sekta hiyo.

Pia imesisitiza dhamira ya serikali kufanya kazi na wadau mbalimbali ili kuimarisha mfumo wa afya.

Waziri wa Afya, Jenister Muhagama amesema hayo leo Novemba 14,2024  wakati wa ufunguzi wa Jukwaa na Maonyesho ya nne  Afya ya Kidigitali na Uvumbuzi  lilnalofanyika Chuio cha Muhas tawi la Mloganzila, Dar es Salaam.

"Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo, sekta binafsi na taasisi za utafiti kuimarisha mfumo wa afya kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi na kwa kukumbatia mabadiliko ya kidigitali na mikakati inayozingatia ushahidi."

Waziri aliongeza kuwa mikakati hiyo itasaidia kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote na kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania wote

Mhagama ameongeza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amepambana na amekuwa kinara  kwenye teknolojia ya kidigitali kwa kuhakikisha mifumo yetu unakuwa ya kidigitali.

"Serikali imeipa kipaumbele teknolojia ya kidigitali ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu tu imeidhinisha kiasi cha shillingi Trilioni 6.2  kuboresha sekta ya afya nchini uwekezaji ambao umejenga miundombinu, mashine za CT scan, Utra sound, MRI, na XRY, 

Akielezea umuhimu wa kukuza utaalamu na utafiti, Waziri Mhagama alisema MUHAS inatoa wataalam wabobezi ambao wamesaidia  kuimarisha huduma za afya nchini.

 "Tunajenga miundombinu ya majengo na kununua vifaa tiba vya kisasa, pamoja na kuimarisha huduma za kibobezi  kwa kutumia teknolojia lengo ni kuhakikisha mnyororo wa huduma za afya  unawafikia watanzania kuanzia uchunguzi hadi matibabu,” amesema  Mhagama.

Aidha amesema amefurahishwa na teknolojia inayotumiwa na Sweden katika  kutoa taarifa za viashiria ya ugonjwa wa saratani ya matiti na kizazi kwa kina mama.

Alisema teknolojia hiyo ina uwezo wa kutoa taarifa za mgonjwa  kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali na kwamba wenzetu wamejipanga kutumia ubunifu huo ili kusaidia utoaji wa huduma za awali kwa wagonjwa wanaobainika mapema kuwa na viashiria vya saratani.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi cha Muhimbili , Prof. Apolinary Kamuhabwa . amesema kuwa Mwaka 2023  Muhas kimekuwa chuo namba tatu barani Afrika na namba moja nchini kwa ubora .

"Chuo chetu kipo tayari kwa ajili ya kuendelea na uandeshaji wa kiteknolojia ya kidigatali na vijana wamekuwa na utashi mkubwa katika matumizi ya Teknolojia. 

"Wanafunzi wa Chuo cha Muhas ikiwa wengi ni vijana wamekuwa vinara wa matumizi wa Teknolojia hasa matumizi ya akili Mnembe nadhani tumeshuhudia kwenye maonesho haya ubunifu wao ".




Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad