HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 22, 2024

MGODI WA UCHIMBAJI WA MADINI GEITA [GGML] YAKABIDHI PIKIPIKI 50 KWA SERIKALI - GEITA

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatarajia kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 224 kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo yanayohusisha kuanza ujenzi wa Ofisi,Vituo na Makazi ya Askari pamoja na kuongeza vitendea kazi vya kisasa kama Pikipiki,Magari,Helikopta na boti hadi sasa Serikali imeshanunua magari 384 kwa ajili ya Jeshi la Polisi pekee. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema hayo wakati akikabidhiwa Pikipiki na Mgodi wa Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu ya Geita (GGML) katika eneo la Bwalo la Polisi Mjini Geita. 

Waziri Mhandisi Masauni ameagiza askari kata waliopewa pikipiki hizo kuhakikisha wanazuia uhalifu hasa kutokana na Mkoa wa Geita baadhi ya waganga kuendesha shughuli za ramli chonganishi na kupelekea kuhatarisha maisha ya watu,hivyo askari hao wametakiwa kuzuia na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana usalama wa raia na mali zao pamoja na kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani.

Makamu wa Rais Mwandamizi wa AngloGold Ashanti Terry Strong baada ya kukabidhi Pikipiki 50 kwa Waziri Mhandisi Masauni amesema kumekuwepo na ushirikiano baina ya Serikali na Mgodi huo na dhumuni ya kutoa Pikipiki hizo ni kwa ajili ya kuendelea kuimarisha usalama wa maisha ya wananchi wa Mkoa wa Geita. 

Martine Shigela,Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema licha ya Mgodi huo kutoa Pikipiki hizo lakini wamekuwa wadau wakubwa wa kutoa misaada mbalimbali katika Mkoa huo na majuzi walikabidhi nyumba 6 za watumishi wa Jeshi hilo kwa Serikali zenye dhamani ya zaidi Shilingi Bilioni 1. 

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Kadogo Venance amesema eneo la kata anayoisimamia ya Bombabili kuna baadhi ya maeneo yana changamoto ya kufikika hivyo uwepo wa Pikipiki aliyokabidhiwa itamrahisishia kufanya kazi yake kwa muda wowote.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad