Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri akizungumza na kuwaonesha waandishi wa habari jinsi wawekezaji wanavyoongezaka nchini. Amezungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo Oktoba Mosi, 2024.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema hali ya uwekezaji nchini kati ya Aprili hadi June, 2024 imeongezeka hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaamy. Amesema kuwa TIC ilisajili Miradi 198 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.69 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi trioni tatu. Pia imetengeneza ajira 9600 nchini.
Amesema kuwa uwekezaji huo ni mkubwa kwa mwaka 2024 ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2023 katika kipindi cha Aprili hadi Juni ambapo ilikuwa miradi 129 wenye thamani dola bilioni moja na ajira 14000
Kwahiyo kwenye hili ongezeko la mitaji kwa asilimia zaidi ya 60, ongezeko la miradi peke yake ni asilimia 53 na ongezeko la matarajio ya ajira ni asilimia 500 na ni hatua kubwa pia ni hatua ya kuvutia mitaji mikubwa kiasi hicho.
"Leo Oktoba Mosi, tumefunga robo ya Tatu ya mwaka 2024, takwimu za awali zinaonyesha ongezeko kubwa zaidi ya uwekezaji katika kipindi hicho.
Haya ni mafanikio na Maendeleo makubwa ambayo yanatokana na Uongozi wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan." Amesema
Jambo jingine Teri amesema mazingira bora ya uwekezaji, kwenye sheria kanunu na taratibu, pia utendaji kazi wa taasisi za serikali ambazo zinasimamia ndio chanzo cha kukua kwa idadi ya wawekezaji nchini.
"Tumpongeze Rais Dkt. Samia Suluhu kwasababu ya uwezo wake kupitia demokrasia ya Uchumi, demokrasia ya kimataifa na kupitia uwezo wake wa uongozi, sera na sheria za nchi za uwekezaji ambazo zinafanya Tanzania kuwa kimbilio kwa wawekezaji." Amesema Teri
Baadhi ya Watendaji wa TIC wakiwa katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba Mosi, 2024.
No comments:
Post a Comment