UJUMBE wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) unazuru nchini Comoro kwa minajili ya utafutaji wa fursa za ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wenyeviti na Watendaji Wakuu ambao ulihimiza Mashirika ya Umma kuangazia fursa nje ya nchi.
Ziara hiyo inafuatia mwaliko wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mheshimiwa Ibrahim Mze na inataratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT,Brigedia Jenerali Petro Ngata.
Mara baada ya kuwasili,Ujumbe wa SUMA JKT ulipata fursa ya kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja na Serikali yake ambapo walimueleza shughuli wanazofanya na Sekta wanazoweza kushirikiana ambazo ni ujenzi,uzalishaji wa bidhaa za chakula na mifugo,madawa na nguo hususan sare.
Aidha,Shirika la SUMA JKT linatoa huduma za ushauri na usimamizi wa miradi,utoaji huduma za katika bandari na elimu.
Shirika la SUMA JKT tayari lina soko la bidhaa nchini Comoro ambapo wanasambaza sare za makampuni ya ulinzi nchini humo.
Kwa upande wake,Gavana wa Kisiwa hicho aliushukuru uongozi wa SUMA JKT kwa kuitikia mwaliko wake na kuwasarifu fursa za kuanza ufuatuliaji.
Ujumbe huo unatarajiwa kuwa na mikutano na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro na pia Sekta binafsi.
No comments:
Post a Comment