SHULE ya awali na msingi New Light ya mchepuo wa kiingereza iliyopo Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imefanya mahafali ya 13 ya kuhitimu darasa la saba ambapo kwa mwaka huu wa 2024 wanafunzi 72 wamehitimu.
Wahitimu wa darasa la saba waliomaliza elimu ya msingi nchini wametakiwa kuishi na kulinda maadili yao wakati huu wanaposubiri kujiunga na elimu ya sekondari ili kuwa na matokeo chanya kwenye jamii.
Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi New Light iliyopo mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Askofu Sommy Severua akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya shule hiyo amesema wanafunzi wanapaswa kuyaishi maadili mema waliyofundishwa.
Mchungaji Sommy amesema wahitimu wa darasa la saba waliomaliza elimu ya msingi nchini wanapaswa kuishi na kulinda maadili yao wakati huu wanaposubiri kujiunga na elimu ya sekondari ili kuwa na matokeo chanya kwenye jamii.
Amesema kadiri miaka inavyozidi kwenda ndiyo maadili yanazidi kuporomoka kwa watoto kufanya au kufanyiwa vitendo visivyompendeza Mungu hivyo wanapaswa kujichunga.
Amesema wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo wamefundishwa maadili mema na bora hivyo wanapaswa kuyaendeleza hayo pindi wakianza elimu ya sekondari mwaka 2025.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Oljoro Namba 5, Lazaro Lesikar Ole Suya amewaasa wahitimu hao kuendelea kusoma kwa bidii na wasiache kusali ili kumuomba Mungu.
Ole Suya amesema amekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Simanjiro Kiria Laizer hivyo atazifikisha baadhi ya changamoto ili zifanyiwa kazi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Israel Maleyeki akisoma risala kwenye mahafali hayo amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanafunzi 14 waliohitimu la saba mwaka 2012.
Mwalimu Maleyeki amesema shule hiyo ina wanafunzi 782 miongoni mwao 72 wamehitimu darasa la saba, kati ya wanafunzi wao 690 ni wa kutwa na 96 wanakaa bwenini.
Mmoja kati ya wahitimu hao, Andrew Lyimo amesema anamshukuru Mungu kwa kufikia hatua hiyo na malengo yake ni kusoma kwa bidii hadi awe rubani wa kuendesha ndege.
Mhitimu mwingine wa shule hiyo Noah Laizer amesema lengo lake ni kuhakikisha anasoma kwa bidii kwenye ngazi ya sekondari na chuo hadi kuwa mhandisi wa barabara.
Mhitimu Emmanuel Laizer ambaye amesema ndoto yake ya kuwa mwanasheria inatimia pindi akimaliza sekondari na kwenda chuo, kwani anatarajia kufaulu vyema masomo yake.
Mhitimu mwingine wa shule hiyo, Hosiana Yohana amesema anamshukuru Mungu kwa kuhitimu darasa la saba na anatarajia kufaulu kwenda sekondari kisha kuwa daktari
No comments:
Post a Comment