Kamishina Msaidizi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha Dkt Remidius Ruhinduka akizungumza wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjadala huo umefanyika leo Agosti 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakichangia mada wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjadala huo umefanyika leo Agosti 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Afisa Uwekezaji Mwandamizi wa UNCDF, Abraham Byamuru, akizungumza wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjadala huo umefanyika leo Agosti 06, 2024 jijini Dar es Salaam.akizungumza wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjadala huo umefanyika leo Agosti 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Mazingira katika Ubalozi wa Uingereza, Catherine Pye, akizungumza wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjadala huo umefanyika leo Agosti 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
WIZARA ya Fedha inathamini maoni ya wadau wa sekta ya nishati safi wanayoyatoa katika kuhakikisha kuwa ajenda ya Mpango wa Taifa wa kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha Dkt Remidius Ruhinduka wakati wa mjadala ulioandaliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), kupitia Mpango wa CookFund na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU, amesema Serikali inadhamiria kuona mpango huo malengo yake yanafikiwa na maoni ya wadau ni sehemu ya utekelezaji wa ajenda hiyo.
Dkt. Ruhinduka imekuja baada ya wito wa wadau wa kuitaka Serikali kupunguza kodi kwenye vifaa vya nishati safi ya kupikia na ikiwezekana kuondoa Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) ili kusaidia watu wengi hasa wasiojiweza kuweza kumudu na kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa.
"Mijadala ya wadau inasaidia katika kukumbushana kuchukua hatua na kuharakisha azma ya Serikali ya kuona asilimia kubwa ya Watanzania wanaachana na matumizi ya nishati chafu ili kulinda mazingira na afya." Ameeleza Dkt.Ruhinduka
Amesema Serikali kupitia sera mbalimbali ikiwemo sera ya Mazingira na Misitu imekuwa ina hamasisha mpango huu na ndio maana Rais Samia alizindua mkakati wa Taifa wa kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo 2034.
"Serikali imeweka mipango mbalimbali ya kimkakati ukiwemo kuhakikisha gharama za ununuzi wa teknolojia ya nishati safi zinapungua ifikapo mwaka 2026.
Lakini pia juhudi nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na kuondoa VAT Katika mitungi yote ya gesi ya asilia ( LPG) inayoingia hapa nchini ili kuhakikisha bei inakuwa nafuu kwa watumiaji." Amesema
Dkt. Ruhinduka
Amesema jitihada nyingine ni pamoja na upatikanani wa huduma za umeme vijijini na ifikapo mwakani 2024 vijiji vyote vitakuwa na umeme.
Kwa Upande wa Afisa kutoka Umoja wa Ulaya (EU) anayehusika na Nishati, Max Peddretti amesema wamefadhili mjadala huo kwa wadau ili kubadilishana mawazo kati ya Serikali na Sekta binafsi na kuona namna utekelezaji wa mpango huo wa taifa utakavyokuwa na mafanikio na kupunguza gharama za upatikanaji wa nishati safi.
Ameongeza kuwa ununuzi wa teknolojia ya nishati safi ni gharama lakini matumizi yake ni rahisi ukilinganisha na matumizi ya mkaa katika mapishi ya kila siku.
Amesema Umoja wa Ulaya unapenda kuona Watanzania wanamudu kununua teknolojia ya nishati safi ikiwemo majiko ya kupikia ili kulinda afya ya watumiaji na kuweka safi mazingira.
Akielezea uzoefu wake katika nchi nyingine zilivyomudu kutumia nishati safi, Catherine Pye, Mkuu wa Idara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Mazingira katika Ubalozi wa Uingereza amesema Uingereza imefanikiwa kwa sababu imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ikiwemo Serikali kutoa umeme wa jua kwa wananchi na ndio maana Serikali yake inasapoti pia mpango huo nchini na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo majiko ya umeme ya kupikia katika shule 200 hapa nchini.
Amesema mjadala huo ungependa kuona vifaa muhimu kama vile majiko ya umeme ( induction) vinapatikana kwa gharama nafuu ikiwa jitihada zitachukuliwa ikiwemo pendekezo kwa Serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama ya kodi na VAT katika vifaa hivyo.
Kwa Upande wa Abraham Byamuru, Afisa Uwekezaji Mwandamizi wa UNCDF ambao ndio wameandaa mjadala huo kupitia ufadhili wa EU amesema lengo ni ksaidia jitihada za Serikali katika mpango mkakati wa miaka 10 wa kutumia nishati safi majumbani na katika taasisi.
Mjadala huo umehusisha wadau kutoka Wizara ya Fedha, wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Kodi (TRA), Shirika la Umeme (Tanesco) na wauzaji wa vifaa hivyo wamekutana ili kujadili utekelezaji wa mkakati huo kwa makanikio zaidi .
“Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, lakini matumizi ya nishati safi kwa kiasi kikubwa yatasaidia kulinda misitu na afya ya watu pia,”
“Tumefurahi kuona Serikali ipo tayari kupokea mapendekezo yetu, lakini imetutaka kuja na tathmini kuona ni fadia gani zitapatikana endapo kodi zitapungua.” amesema.
No comments:
Post a Comment