Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muungano Kata ya Goba, Bw. Lazaro Sentimoja akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kulangwa Bw. Emmanuel Tito msaada wa madawati uliotolewa na kikundi cha Wanawake Jeshi Kubwa wa Mtaa Kulangwa Kata ya Goba ,Wilayani Ubungo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake Jeshi Kubwa Frida kasomangala akionyesha hati ya shukrani waliyokabidhiwa.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kulangwa Bw. Emmanuel Tito (kulia) akimshukuru Mwenyekiti wa Mwanawake Jeshi Kubwa. Bi. Frida Kasomangala mara baada ya kupokea msaada wa madawati 30 ya Shule hiyo.
Picha ya pamoja viongozi wa kundi la kina mama Jeshi Kubwa na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Muungano pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi kulangwa.
madawati yaliyokabidhiwa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muungano,Bw. Lazaro Sentimoja akiwashukuru Kikundi cha Wanawake Jeshi Kubwa baada ya kupokea Msaada wa Madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Kulagwa iliyopo Goba Mtaa wa Muungano.
KIKUNDI cha Wanawake Jeshi Kubwa kutoka Goba Kulangwa kimetoa msaada wa madawati 30 yenye thamani ya Shilingi Milioni tatu(3,000,000/)kwa Shule ya Msingi Kulangwa iliyopo Kata ya Goba, Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akimkabidhi madawati hayo katika hafla iliyofanyika Agosti 13,2024 katika Shule hiyo, Mwenyekiti wa kundi hilo Bi Frida Kasomangala amesema madawati hayo yametokana na michango ya kina mama ikiwa ni majitoleo kwa jamii.
Amesema kundi la Wanawake Jeshi Kubwa linaundwa na Wanawake 79 wenye makazi ya kudumu na limekuwa likitoa msaada kwa jamii ikiwemo vituo vya Watoto wenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya kurudisha shukuruni Kwa Mwenyezi Mungu.
"Sisi Wanawake Jeshi Kubwa tumekuwa tukichangishana fedha na kuangalia mahitaji ya jamii ili kutatua au kupunguza changamoto inayowazunguka hivyo msaada wa madawati itatatua tatizo la upungufu wa madawati shuleni hapa.Alisisitiza Bi. Kasomangala.
Awali akisoma risala ya kikundi hicho ,Makamu Mwenyekiti wa Wanawake Jeshi Kubwa Bi. Macklina Magutu alisema kundi hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Muungano katika kuchangia maendeleo ya eneo hilo.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muungano, Bw. Lazaro Sentimoja amelishukuru kundi la Wanawake Jeshi Kubwa Kwa msaada waliotoa hasa katika kutatua changamoto za uhaba wa madawati Kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi kulangwa na kuomba vikundi vingine kuiga mfano Kwa kujitolea Kwa jamii.
Akishukuru kwa niaba ya Wanafunzi Shule hiyo Mwanafunzi Angel Francis wa darasa la Saba ameshukuru Jeshi Kubwa kwa kuwaletea madawati na kuomba msaada huo usiishie hapo wazidi kusaidia kumaliza changamoto hiyo.
" Tunawashukuru sana Kwa kutuletea madawati tunaomba mzidi kutusaidia kwani bado tunauhitaji wa madawati" Alisisitiza Angel.
Halfa hiyo ya kukabidhi madawati ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa elimu kutoka Halmashari ya Wilaya ya Ubungo, ofisini ya Diwani pamoja na Serikali ya Mtaa wa Muungano.
No comments:
Post a Comment