Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba leo tarehe 13/08/2024 katika ofisi za makao makuu ya TET jijini Dar es salaam ameongoza kikao cha wajumbe wa menejimeti na ujumbe wa Taasisi ya elimu ya nchini Malawi kikao kilichokuwa na lengo la nchi ya Malawi kujifunza juu mabaoresho ya mtaala yaliyofanyika ya mwaka 2023.
Katika kikao hicho ujumbe wa Malawi uliongozwa na Mratibu wa Mitaala ya elimu ya msingi katika Taasisi ya Elimu ya Malawi, Bw. Michael Simawo ambaye amesema kuwa lengo la ziara yao ni kutaka kufahamu namna Tanzania imefanya maboresho ya Mtaala wa elimu.
“Tumefurahia kufika Tanzania na kufahamu masuala mbalimbali yahusuyo mfumo wa limu nchini ambapo tulianzia Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia na sasa tumemaliza hapa TET ili tujifunze zaidi kwani tuko kwenye harakati za kuboresha elimu yetu,“amesema Bw. Simawo.
Amesema kuwa, wako katika hatua za mwisho za maboresho ya Mitaala ya elimu hivyo wakaona ni vyema wapite katika nchi mbalimbali wajifunze ikiwemo Tanzania ambayo imefanya maboresho ya mitaala hivi karibuni.
Kwa upande wake, Dkt. Komba amesema kuwa ni jambo jema kwa nchi ya Malawi kuweza kujifunza juu ya Mitaala ya Tanzania, na kwamba ni jambo jema kupata uzoefu wa nchini nyingine ambao utasaidia katika kuboresha elimu yao.
Katika kikao hicho, Dkt. Komba alipata nafasi ya kuwaelezea hatua mbalimbali zilizopotiwa katika maboresho ya mitaala ya Elimu yaliyofanyika na namna yalivyoanza kufanyika katika baadhi ya ngazi ya madarasa nchini.
Pia ujumbe huo wa Malawi ulipata nafasi ya kujionea darasa janja (Smart class) namna linavyofanya kazi kwa wakati mmoja inapoweza kutumika kufundishia na kijifunzia kwa walimu zaidi ya 300 na kuangalia studio za kurekodi sauti na video mbalimbali za kielimu.
Tuesday, August 13, 2024
Home
Unlabelled
TET AONGOZA KIKAO CHA WAJUMBE WA MENEJIMENTI NA UJUMBE WA TAASISI YA ELIMU MALAWI
TET AONGOZA KIKAO CHA WAJUMBE WA MENEJIMENTI NA UJUMBE WA TAASISI YA ELIMU MALAWI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment