HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 6, 2024

NIRC:Sheria ya Umwagiliaji imetungwa katika kuondoa changamoto ya Umwagiliaji

 


Na Chalila Kibuda,Dodoma 

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) imesema sheria ya umwagiliaji imewekwa katika  kuondoa changamoto  zinazoikabili sekta ya umwagiliaji nchini.

Akizungumza leo kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma Afisa Sheria mwandamizi NIRC Amina Mweta  amesema  kumekuwa na ushiriki mdogo wa wakulima na sekta binafsi katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ni chanzo cha uanzishwaji wa sheria hiyo itayofanya shughuli za umwagiliaji kuwa endelevu nchini kutokana na uzalishaji wa Sekta hiyo.

"Sheria ya Taifa ya umwagiliaji na.4 ya mwaka 2013 imetugwa na kupitishwa na bunge mwaka 2013 ikatiwa saini na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Oktoba  20,2013 sheria hii imeanzishwa na Tume ya Umwagiliaji ili kusimamia kilimo cha umwagiliaji na kutatua changamoto za wakulima",Amesema.

Ameongeza kuwa sababu nyingine ya kuanzishwa sheria hiyo ni pamoja udhaifu wa mifumo ya kitaasisi ambao ulikua haukidhi kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji lakini pia uvamizi wa maeneo ya ardhi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Sambamba na hayo amebainisha vitendo vilivyokatazwa katika sheria ambapo ni pamoja na kuingia katika ardhi ya umwagiliaji kwa madhumini tofauti na umwagiliaji. 

Amesema ,kuruhusu sumu ya viwandani au uchafu wa majumbani kuingia kwenye skimu yeyote ya umwagiliaji bila kutibu maji kikamilifu kunaua uoto wa asili pamoja na umwagiliaji huo kukosa tija kwa Taifa.

Aidha amesema kutokana na hali iliyokuwepo na changamoto ambazo zimeikabili sekta ya umwagiliaji sheria imesaidia kuongezeka kwa mchango wa umwagiliaji katika uzalishaji wa chakula na lishe lakini pia kuongezeka kwa pato la wakulima na Taifa kwa ujumla.

Naye Mhandisi Mwandamizi wa Umwagiliaji  Naomi Mcharo amesema kwa mwaka huu wa fedha NIRC wamejipanga kuchimba visima 1000 nchi nzima.

Aidha amesema NIRC wanaendelea na miradi mbalimbali ya umwagiliaji nchini ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na kumnufaisha mkulima

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad