Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Wakulima,Wafugaji pamoja na Wavuvi kutumia Pembejeo zenye wakati alipotembelea Mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma
Katika kulinda ubandia wa bidhaa na kuua mitaji
Na Chalila Kibuda ,Dodoma
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC) William Erio amesema kuwa wajasiriamali kutengeneza vifungashio vyenye ubora katika kulinda soko kwa ambao watafanya bandia Biashara zao.
"Ubora wa bidhaa yeyote isipolindwa na kufanyika bandia yake kunafanya mfanyabiashara kurudi nyuma kutokana na maarifa na fedha aliyiwekeza kuwa kazi bure" amesema Erio.
Hayo ameyasema leo mara baada ya kutembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Kilimo Kilimo Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema katika Maonesho ya Nane Nane Wakulima wanatakiwa kuhakikisha wanatumia Pembejeo zenye ubora ili waweze kulima kwa faida na kukuza uchumi wa nchi kutokana na mazao kuwa na soko ndani na nje ya nchi.
Amesema FCC imeshiriki maonesho kwa lengo kuu la kutoa elimu kwa Wakulima,Wafugaji pamoja na Wavuvi juu ya namna bora ya kumlinda mraji.
"Tumeshiriki kwenye maonesho haya ili kutoa elimu kwa wadau wote wa kilimo kuepuka matumizi ya bidhaa bandia ikiwemo pembejeo za kilimo ili kuhakikisha wanazalisha mazao yenye ubora",Amesema Erio.
Aidha amesema pia katika maonesho hayo wanawashauri wazalishaji kufungasha bidhaa zao kwa kutumia viwango vilivyothibitishwa na Shirika la viwango la Tanzania (TBS).
Sambamba na haya Erio ametoa wito kwa wananchi na wakulima wote nchi kuhakikisha wanajiandikisha kwenye daftari ya kudumu la wapiga kura ili kushiriki uchaguzi wa serikali na kuchagua viongozi watakao wasaidia kuendeleza kilimo na kuwatafutia masoko ya uhakika.
Amesema kauli mbiu ya maonesho hayo inachochea wakulima kupata viongozi ambao watasaidia kupeleka agenda zao lakini kuwafanikisha kupata masoko Duniani kote.
"Kauli mbiu ya maonesho kwa mwaka huu 'Chagua viongozi bora wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo,mifungo na Uvuvi' imekuja wakati mwafaka tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na serikali kuu hivyo nitoe rai kila mtu alifikisha umri wa kujiandikisha akajiandikishe",Amesema Erio.
No comments:
Post a Comment