Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa akikabidhi viti Viongozi wa UWT wa kata za wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Agosti 05, 2024.
Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa akizungumza na Wanawake wa UWT leo Agosti 05, 2024 wakati wa kukabidhi vitio 360 katika wilaya ya Ilala jijini Dra es Salaam.
Baadhi ya Viti vya kata za Wilaya ya Ilala.
Baadhi ya Wananwake wa Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) wakiwa katika mkutano wa makabidhiano ya Viti 360 vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa leo Agosti 05, 2024 jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MBUNGE wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi Taifa (UWT) (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa leo Agosti 05, 2024 ametoa viti 360 katika kata za wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kwenda kuziba pengo lililopo katika ofisi za kata.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi viti hivyo, Stella amesema lengo la kutoa viti hivyo kama kitendea kazi kwaajili ya wajumbe na mtu yeyote anayefika katika ofisi yakata kupata huduma asipate tabu namna ya kukaa.
“Kama mnavyojua kwa sasa shughuli ni nyingi kama wanachama kuja kuchukua fomu, kujiandikisha hivyo nimetoa ili kusaidia jumuiya ya UWT kwenye ngazi ya kata.” Amesema
Licha ya hayo Stella ametoa wito kwa viongozi wa UWT kuendelea kuhamasisha watu waende kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura pia kwa wananchi amewaomba wajitokeze kujitokeza kwenye daftari hilo na wakati wa uchaguzi wajitokeze kupiga kura.
Mbunge Stella amewaomba UWT kuendelea kuyatangaza yale mema yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumuungano mkono kwa yale anayoyafanya.
“Kwa wale ambao wamesahau tuendelee kuwakumbusha kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya 1, 2, 3, 4…..” Amesisitiza
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wa Chama cha Mapinduzi Tifa (UWT) Wilaya ya Ilala, Neema Kiusa ametoa wito kwa UWT kuelekea uandikishaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura kutoa hamasa kwenye kata, kwenye wilaya ili kila mmoja aweze kujiandikisha pale ifikapo mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu.
“Wilaya ya Ilala inamajimbo matatu na jimbo lenye watu wengi ni jimbo la Ukonga, sisi kama viongozi ipo mipango mikakati ya Kwenda kuwafikia viongozi wote pamoja na kufikia makundi yote hasa makundi maalumu, mama na baba lishe na wasusi kuwafikia kwaajili ya kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandiskisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.” Amesema Neema
Kwa upande wa wawakilishi wa UWT wamemshukuru Mbunge wa Viti Maalum Umoja wa Wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa kwa kuona changamoto iliyopo katika ofisi za kata na kuweza kutoa msaada wa viti.
“Tunashukuru Sana sana kwa kutupatia viti hivi, vitakwenda kutusaidia katika vikao vyetu vya utendaji katika kata zetu, pia vitasaidia wananchi mbalimbali wataofika katika kata zetu kupata huduma mbalimbali.”
No comments:
Post a Comment