HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 5, 2024

AIRTEL WAMKABIDHI PIKIPIKI MSHINDI WA PROMOSHENI YA UPIGE MWINGI

 Meneja wa uhusiano na Mawasiliano Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akimkabidhi Shabani Ramadhani mshindi ufunguo wa pikipiki mara baada ya kuibuka mshindi wa  promosheni yao ya upige mwingi iliyofanyika kwa miezi mitatu. kampeni hiyo imehitimishwa leo Agosti 05, 2024 kwa kumkabidhi mshindi huyo pikipiki. Kulia ni Meneja Airtel Money Makao Makuu, Janeth Kwilasa. Mshindi wa promosheni ya upige mwingi na Airtel, Shabani Ramadhani akionesha ufunguo mara baada ya kukabidhiwa leo Agosti 05, 2024 jijini Dar es Salaam. katikati ni Meneja wa uhusiano na Mawasiliano Airtel, Jackson Mmbando  na kulia ni Meneja Airtel Money Makao Makuu, Janeth Kwilasa 


KAMPUNI ya Airtel imemkabidhi mshindi pikipiki kwenye promosheni yao ya upige mwingi iliyodumu kwa takribani miezi mitatu.

Nia ya kutoa zawadi hiyo  kuwawezesha watanzania kuweza kuishi ndoto zao na kuinga serikali mkono.

Meneja wa uhusiano na Mawasiliano Airtel, Jackson Mmbando akizungumza wakati  wakikabidhi zawadi hiyo jijini Dar es salaam leo,  Agosti 5 ,2024 na kuongezea kuwa promosheni hiyo ilikuwa ikitoa zawadi tofautitofauti kama Dakika, simu za mkononi pamoja na vifurushi vya Intaneti.

Aidha Jackson amesema serikali imeweka mazingira ya watu wengi kufanyabiashara mtandaoni hivyo wao kama kampuni wanaamini bando walizopata watatumia kufanyabiashara za mtandaoni na zawadi hizo wamejishindia watu kutoka mikoa mbalimbali ya nchi.

Kwa upande wa Meneja Airtel Money Makao Makuu, Janeth Kwilasa  amesema promosheni hiyo imewasaidi watanzania wengi wanaotumia mtandao huo na nia yao ni kurudisha walichokipata kwa watumiaji wa mtandao huo.

Mshindi wa pikipiki wa promosheni hiyo Shabani Ramadhani amesema promosheni ya pikipiki hiyo itamsaidia kutimiza malengo yake ya kibiashara.

Kampeni hiyo imedumu kwa miezi mitatu na siku ya leo imefika tamati .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad