Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhe.Gerald Geofrey Mweli akikabidhi nyaraka muhimu za jengo jipya la maabara ya TPHPA Kibaha Pwani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPHPA Profesa Andrew Temu katika tukio lililofanyika leo Agosti 13, 2024 kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Profesa Joseph Ndunguru.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Mhe.Gerald Geofrey Mweli akishuhudia wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TPHPA Profesa Andrew Temu akikabidhi nyaraka muhimu za jengo jipya la maabara ya TPHPA Kibaha Pwani kwa Mkurugenzi Mkuu wa maabara hiyo Profesa Joseph katika hafla iliyofanyika leo Agosti 13, 2024.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Mhe.Gerald Geofrey Mweli akikabidhiwa nyaraka muhimu za jengo jipya la maabara ya TPHPA Kibaha Pwani na Casmil Musobi Mkurugenzi wa kampuni ya ushauri ya Digital Space kushoto anayepiga makofi ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPHPA Profesa Andrew Temu.
KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo Mhe.Gerald Geofrey Mweli ameipongeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA) kwa kuokoa tani milioni 1.1 za nafaka kwa kudhibiti Kweleakwelea waliovamia halmashauri 24 nchini.
Ameeleza hayo leo Agosti 13, 2024 wakati wa kukabidhi jengo la Maabara mpya ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) lililopo Kibaha mkoani Pwani.
"Kwa hesabu hizi rahisi tani hizi za chakula ukipiga hesabu vizuri utaona ni jinsi gani TPHPA wamechangia katika kuboresha usalama wa chakula na kuokoa tani 500 za nafaka yakiwemo mahindi.Pia amesema pesa za ujenzi zimetolewa na serikali na wadau mbalimbali pamoja na mikopo na sisi kama wizara ya kilimo na TPHPA tunatakiwa kuzirudisha fedha hizi kwa njia tatu ikiwemo kuhakikisha kuna usalama wa chakula, kuimalisha biashara ya kimataifa kwani biashara hiyo italeta fedha nyingi za kigeni.
Mradi huu utatumika kulinda mazao yote ya nafaka, hivyo niseme wazi kuwa tumeanza safari ya uhakika ya kuhakikisha tunaingia kwenye soko la chakula la Duniani,"amesema Kweli.
Amesema tusipojiandaa vya kutosha tutazalisha chakula na tutabaki nacho hapa nchini,lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa AGRFA alisema anataka kulisha duniani na tulichangua mazao saba ya nafaka hivyo tujivunie tunachozalisha kwa kuthamini mchango wa maabara ya TPHPA.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Andrew Temu anasema kituo hicho ni muhimu katika kuendeleza kilimo na mazao yake kwani Dunia kwa sasa inaendelea kupunguza matumizi ya viuatilifu kwenye baadhi ya maeneo.
"Katika hili tutatumia bio control na huu ni mchango mkubwa sana kwetu presha kubwa nilizozipata kutoka kwa jamii kipindi Cha uongozi wangu ni namna ya kuondoa changamoto hizo katika mazao yote kwa kutumia vituo hivi vya kisayansi vya utafiti,"anasema Profesa Temu
Ameongeza kuwa wao kama TPHPA wameiona hiyo fursa na wataifanyia kazi kwa kuzingatia miundo mbinu iliyopo imeendelea kuboresha shughuli zao za kuutafiti ili kukikuza kilimo hivyo Usimamizi mzuri wa Kituo hicho utazingatiwa kwa kuhakiki ubora wa viuatilifu nchini kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi.
Aidha,Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Nduguru akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo anasema makabidhiano ya maabara hiyo yataboresha huduma za uthibiti viuatilifu kwa njia ya kibaiolojia ili kupunguza matumizi ya viuatilifu vyenye sumu kali katika Mimea na kulinda afya za walaji,wanyama pamoja na mazingira.
Akifafanua zaidi moja ya majukumu ya maabara hiyo katika zao la mahindi amesema Udhibiti wa gugu aina ya Kiduha na Funza wa mabua katika zao la Mahindi kwa kutumia teknolojia ya sukuma vuta (Push pull technology): Mwaka 2016 hadi 2019 tekinolojia hii ilisambazwa katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Arusha ambapo Udhibiti huu ulifanikiwa kwa zaidi ya 65%
Udhibiti wa Nondo mgongoalmasi (Diamond backmoth) ambao ulwanashambulia mazao jamii ya kabichi kwa zaidi ya 65%. Wadudu hawa walidhibitiwa na nyigu aina ya Diadegma Semiclausum kati ya mwaka 2002 hadi 2005 kwa 70% katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Iringa.
Amefafanua kuwa kati ya Mwaka 2020 hadi 2023 kituo hicho pia kimesajili jumla ya Viuatilifu hai 22 kama ifuatavyo Wadudu marafiki 10, Kuvu (fungi) 9, Bacteria 2 pamoja na Plant Extract 1
Pia Profesa Nduguru anasema katika bajeti ya Mwaka 2023/2024 wametenga zaidi ya Milioni 300 kwa ajili ya kuwezesha shughuli za kituo hicho kwa kununua vifaa vya maabara na kuendelea kufanya utafiti mbalimbali.
No comments:
Post a Comment