Katika Banda la Wizara ya Afya huduma mbalimbali zinatolewa kuanzia Elimu ya Afya, Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa, Chanjo dhidi ya Homa ya ini, Uviko 19, pamoja na Chanjo dhidi ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya Kizazi kwa wanawake
Katika dawati letu la elimu na uhamasishaji tuna wataalam wa masuala ya Afya ya Akili, Lishe na Tiba Asili. Kwenye dawati hili pia utapata elimu ya Ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi pamoja na huduma za upimaji VVU, Kifua Kikuu, na hapa tuna Maabara tembezi ambayo ina vifaa vya kisasa vya upimaji na wataalam wetu watakupima ewe mwananachi na kubaini endapo una maambukizi ya TB.
Tunatoa huduma za uchunguzi wa awali wa Saratani ya Malngo wa Shingo ya Kizazi kwa wanawake, Saratani ya Matiti, Huduma za Uzazi wa Mpango njia zote zinapatikana.
Huduma hizi zote zinatolewa bureee! Hima kwako mwananchi kuchangamkia maonyesho haya uweze kupata huduma hizi muhimu za afya.
Tunazo pia Taasisi zetu zilizo chini ya Wizara ya Afya zikiwemo, Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI, Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali GCLA, Hospitali ya Benjamin Mkapa BMH, Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba TMDA, pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ambao pia wanatoa huduma katika maonyesho haya.
No comments:
Post a Comment