DMI ni moja ya taasisi zilizopo katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Timu ya wataalam kutoka chuo Cha Bahari Dar es Salaam -DMI wanaendelea kutoa elimu ya masuala ya ubaharia pamoja na fursa zinazopatikana baharini.
Aidha chuo Cha Bahari Dar es Salaam -DMI kinawakaribisha wananchi kutembelea kwenye Banda lao lililopo ndani ya KARUME HALL.
Huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na usajili wa wanafunzi wanaojiunga na Kozi za Cheti na Diploma bila malipo yoyote pamoja na elimu ya Ubaharia.


No comments:
Post a Comment