HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2024

Masauni awataka Askari kuvitendea Haki Vyeo

 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi hati ya kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi, baada ya kula kiapo kuwa mjumbe wa tume, leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WAZIRI  wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amewataka Askari na Maafisa wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo kutenda kazi kwa kufuata haki na uadilifu katika kuwahudumia wananchi baada ya Askari na Maafisa hao kupandishwa vyeo na Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Ameyasema hayo,leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji ambapo kwanza amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa upandishaji huo ambao ulikoma takribani kwa miaka mitano.

‘Ni Imani yangu sasa kwamba mashauri yote yaliyokuwa hayajashughulikiwa sasa tume itaweza kuyashughulikia lakini sasa niungane na Mkurugenzi wa Tume hii kumshukuru sana Amiri Jeshi Mkuu,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa upandishaji vyeo ambao aujaacha askari hata mmoja kuanzia ngazi ya chini mpaka juu sasa nendeni mkavitendee haki vyeo hivyo,haki uenda na wajibu naombeni mkawe waadilifu na mkafanye kazi alizokusudia Mheshimiwa Rais ya kuzuia na kupambana na uhalifu,huko chini vilio ni vingi nendeni mkavisikilize na mvitafutie ufumbuzi’.alisema Waziri Masauni

Akizungumzia moja ya changamoto alizokumbana nazo wakati akifanya ziara katika vyombo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo aligusia hoja iliyoibuliwa na askari mbalimbali wa Jeshi la Magereza waliokua wakiulizia zoezi la upandishaji vyeo ambalo ulipita muda mrefu bila kupandishwa vyeo na sasa anashukuru kuona hoja hiyo imefanyiwa kazi.

Akizungumzia zoezi hilo la Upandishwaji vyeo Mkurugenzi Msaidizi wa tume hiyo,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,George Mwansasu alitaja idadi ya waliopandishwa vyeo,Jeshi la Polisi Maafisa Wandamizi waliopandishwa ni 154,Zimamoto na Uokoaji Maafisa Wandamizi 11,Jeshi la Uhamiaji waliopandishwa ni Maafisa Waandamizi 50 na Jeshi la Magereza waliopandishwa ni 50.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa wizara hiyo,Miriam Mmbaga akiweka wazi juu ya kuongezeka kwa ufanisi wa utendaji kazi baada ya kuongezeka kwa rasilimaliwatu ambayo katika vyombo vya usalama upandishwaji vyeo huo unaendana na utoaji na usimamizi wa majukumu katika shughuli zao za kila siku.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi hati ya kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, Mkurugenzi Msaidizi wa tume hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, George Mwansansu, baada ya kula kiapo kuwa mjumbe wa tume, leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga (kulia), Kamishna wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Jeshi la Magereza, Jeremiah Katungu (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, (hayupo pichani) wakati akiongoza Kikao cha Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kushoto), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan (katikati), Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza (kulia) wakifuatilia mjadala wakati wa Kikao cha Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad