HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 30, 2024

TBS YAWATAKA WAFANYABIASHARA NA WATOA HUDUMA KUTUMIA VIPIMO KWA USAHIHI

NA MWANDISHI WETU

Katika kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara,watoa huduma pamoja na wananchi kutumia vipimo kwa usahihi ambapo itasaidia kukabiliana na changamoto za kimazingira,kijamii pamoja na kiuchumi kwa lengo kuepusha madhara yanayosababishwa na kutotumia Vipimo kwa usahihi.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 30,2024 Jijini Mbeya na Mwenyekiti wa Bodi TBS, Prof. Othman Chande wakati wa kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo yamefanyika Jijini humo.

Prof. Chande amesema vipimo ni msingi wa maendeleo kwani vinatupatia takwimu na taarifa muhimu zinazohitajika ilikufanya maamuzi sahihi ili kuendeleza uvumbuzi na hatimae kuhakikisha maendeleo endelevu kwa jamii.

Aidha amesema Metrolojia ni sayansi muhimu hususani kwenye kukabiliana na changamoto za kimazingira ambapo ikitumika kwa usahihi itasaidia kuepukana na majanga na kuepusha vifo vya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa.

"Mfano taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewaili kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo kimbunga,mafuriko na mengineyo haya yote yanategemea usahihi wa vipimo"amesema Prof. Chande.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa tukio hilo la maadhimisho linatumika kama jukwaa muhimu katika kukuza uelewa kwa watu mbalimbali kuhusiana na masuala yanayohusu vipimo na kushughulika ambapo itachagiza uelewa wa kukabiliana na changamoto za kimazingira,kijamii na kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Upimaji na huduma za Metrolojia, Ridhiwani Matange amesema usahihi wa vipimo inahitajika katika maisha ya kila siku ya mwanadamu mathalani katika afya kuanzia katika manunuzi ya chakul,uandaaji wa chakula pia katika ulaji.

"Kwenye kilimo ubora wa pembejeo za kilimo,ubora wa udongo,mashine za kilimo,na hata uuzaji wa mazao ya kilimo hicho vipimo sahihi vinahitajika"amesema.

Aidha amesisitiza matumizi ya nishati mbadala na kuachana na kukata miti na kuchoma mkaa wakati dunia inapofanya jitihada za kupunguza matumizi ya mafuta na kubadili mifumo ya magari kuwa ya umeme,gesi na pengine maji.

MAADHIMISHO hayo ya siku ya Vipimo duniani hufanyika kila mwaka Mei 20,2024 na kitaifa yamefanyika Leo Mei 30,2024 Jijini Mbeya na yamebeba kauli mbinu isemayo 
"Tunapima leo kwa kesho endelevu" ambapo TBS kama chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia vipimo imekua ikisimamia ikihakisha vipimo vinazingatiwa kwa lengo la kuimarisha ubora,wa huduma na maisha Bora kwa wananchi.

















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad