HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 25, 2024

NBAA YAWAFIKIA TANGA

 Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inawakaribisha wananchi kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024 yenye kauli mbiu isemayo "Elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani" yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Uhusiano na Mawasiliano Magreth Kageya amesema wanatoa huduma zote ikiwemo kutoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili kwa ajili ya kufanya Mitihani, maelezo juu ya ulipaji wa ada mbalimbali na pia ametoa wito kwa wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA.

Pia amesema lengo kuu ni kutoa Elimu na uelewa juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NBAA

Amesema baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha maonesho ya elimu ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya Kihasibu na Kikaguzi.

Pia amesisitiza kuwa Bodi hiyo kwa sasa inatumia mifumo ya kidijitari kutoa huduma zake kwa kupitia tovuti yao hivyo amewasisitiza wananchi kutembelea tovuti ya Bodi hiyo ya www.nbaa.go.tz.
Wafanyakazi wa NBAA wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda la Bodi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024 yenye kauli mbiu isemayo "Elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani" yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yanayofanyika jijini Tanga yaliyoanza tarehe 25 hadi Mei 31, 2024
Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiomoni wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa akitoa elimu kwa wananchi walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Macechu wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Maafisa kutoka NBAA Hassan Kawambwa (wa kwanza kushoto) pamoja na Majura Kafumu wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024
Maonesho yakiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad