HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 22, 2024

Mwanga Hakika Bank yazindua huduma ya mikopo kwa wajasiriamali ‘Fursa Loan’

 
· Wajasiliamali wadogo na wa kati kupata mkopo wa Fursa wenye gharama nafuu na dhamana rahisi zinazolingana na aina ya biashara zao

· Huduma hiyo inakuja na akaunti ya malengo ili kuwasaidia kuhifadhi pesa kwa urahisi

Dar es Salaam. Katika azma yake ya kuwezesha biashara nchini, Benki ya Mwanga Hakika imeleta sokoni huduma ya mikopo rahisi kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuwakwamua kiuchumi ijulikanayo kama Fursa Loan.

Huduma hiyo ya kipekee inakuja wakati ambapo watanzania wengi wamekuwa wakihitaji huduma za mikopo yenye riba nafuu na dhamana zinazoendana na aina ya biashara zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, leo Jumatano 22 Mei, 2024, Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa Mwanga Hakika Bank, Mwinyimkuu Ngalima alisema benki hiyo imejizatiti katika kuleta huduma zinazokidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya wateja.

“Tunafarijika kuja na huduma hii ya mkopo kwa wajasirimali wadogo na wa kati ambayo ni mikopo yenye gharama nafuu na dhamana zake zinalingana na aina ya biashara zao.

“Tunaamini huduma hii inaenda kuwa msaada mkubwa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kama mamalishe, bodaboda, madereva tax na wengineo ambao wamekuwa wakishindwa kupata mikopo kutokana na gharama kubwa na kutokuwa na dhamana,” alisema.

Ili mteja aweze kupata mkopo kwenye benki anahitaji kuwa na dhamana ya mali isiyohamishika kama vile nyumba zenye hati miliki au mashine (kiwanda) jambo ambalo limekuwa likiwakosesha mikopo hasa wafanyabiashara wadogo wasio na dhamana hizo.

Huduma hii inatoa fursa ya kipekee kwa wafanyabiashara wadogo n awa kati kupata mikopo yenye gharama nafuu na dhamana rahisi itakayowawezesha kuongeza mitaji kwenye biashara zao ili ziweze kukua zaidi.

“Tunawakaribisha wajasiriamali wote bila kujali aina ya biashara kutumia fursa hii ili waweze kukuza biashara zao kwa kuongeza mitaji,” alisema.

Tanzania inakadiriwa kuwa na biashara ndogondogo na za kati takribani milioni tatu zinazochangia pato la taifa kwa asilimia 27. Pia, sekta hii ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu nchini ikichangia katika ajira na ubunifu.

Mteja anaweza kupata huduma hii kupitia tawi lolote la Mwanga Hakika Bank nchini.

Ili kuipa thamani zaidi, benki hiyo imekuja na huduma ya ziada ya akaunti ya malengo (Fulsa saving account) itakayowawezesha wafanyabiashara wadogo kutunza pesa kwa malengo ya baadaye.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad