HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 14, 2024

IDADI YA WANAWAKE WANAOENDA KUPATA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO YAONGEZEKA

 


KWA kipindi cha mwaka 2023-2024 idadi ya wanawake wanaoenda kuhudhuriaa klinic kwa ajili ya kupata huduma za njia za uzazi wa mpango wa muda mrefu imeongezeka kutoka 6500 hapo mwanzo hadi kufikia wanawake 18750 hii ikiwa ni matunda ya  mradi wa kuimarisha vituo vya umma unaotokelezwa na shirikia la Mariestopes  ambao umewezesha mafunzo kwa watoa huduma za afya na watoa huduma ngazi ya jamii. .

Mratibu wa huduma  wa afya ya baba, mama na mtoto wilaya ya Igunga Shekha Ally alisema kuwa hili ni ongezeko kubwa sana ukilinganisha na idadi ya vituo vilivyopo ambavyo ni vituo 70 tu katika wilaya ya Igunga.

Kwa idadi hii bi shekha ameishukuru Marie Stopes kwakuendelea kuwawezesha watoa huduma, ufuatiliaji pamoja na kuratibu vikao elekezi ambapo imesaidia  kuongeza uwezo kwa watoa huduma hao.

Leonard Charles baba wa watoto wawili amesema kuwa elimu ya uzazi wa mpango imemnufaisha pakubwa kutokana na kuweza kuwazaa watoto kwa kuachanisha iliyofanya aweze kuendesha maisha kirahisi kutokana na kuwa na idadi ya watoto anaowamudu kuwalea kwa wakati huu lakini pia mke wake na Watoto hao wakiwa na afya njema .

Tunapokutana kwenye vikao vyetu huwa tunaelimishana, uzazi wa mpango hata sisi wanaume tunatumia hasa matumizi ya kinga (kondomu) ambayo inazuia mimba zisizotarajiwa pamoja na magonjwa ya ngono" alisema leonard.

Aidha aliongeza kuwa ni muhimu kwa wanaume kuhusishwa katika masuala ya afya ya uzazi ili wasaidie wakina mama kupanga idadi ya watoto kwa manufaa ya watoto na mama mwenyewe kuwa na afya njema.

"Nadhani ni muhimu kwa kina baba kushiriki uzazi wa mpango kwasababu mama anapokuwa anazaa hapa na hapa watoto wanakuwa hawana afya ile nzuri cha pili mama anadhohofika ki afya"alisema Leonard.

Jonesta Mhagama muuguzi mkuu katika kituo cha afya Simbo amesema kuwa kupitia mafunzo hayo ameweza kujiamini na kuongeza uwezo katika kutoa huduma za afya ya uzazi. 

Marie Stopes kupitia mradi wake wa kuwezesha vituo vya afya vya umma imeweza kutoa vifaa mbalimbali , mafunzo kwa watoa huduma na kuratibu vikao shirikishi vya ufatiliaji  kwa kushirikiana na uongozi  na kamati za afya wilaya ya Igunga .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad