HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 20, 2024

CHINA IKO TAYARI KUONGEZA MISAADA KWA TANZANIA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Ushikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (CIDCA) Bw. Luo Zhaohui walipokutana kwa mazungumzo Ofini kwakwe jijini Beijing, China.

 Mkutano ukiendelea

CHINA imesema itaendelea kufadhili miradi mipya ya kimkakati ya Tanzania inayoendelea, baada ya kuridhishwa na utekelezwaji ya miradi ya awali.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Misaada la China (CIDCA), Luo Zhaohui, aliyasema hayo kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, yaliyofanyika jijini Beijing, China mwishoni mwa wiki.

Zhaohui alisema kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaweza kusaini mikataba mipya ya ushirikiano na misaada Septemba mwaka huu pembezoni mwa mkutano wa Wakuu wa Nchini na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) ambao amealikwa tayari.

"Tumesikia maelezo yako ndugu Waziri na nikuahidi kwamba tutafadhili hatua ya pili ya miradi inayoelekea kukamilika awamu ya kwanza na mingine ambayo umeiomba tunaweza hata kusaini wakati Rais wako atakapokuja Septemba mwaka huu," alisema Zhaohui.

CIDCA ndiyo taasisi inayopitisha misaada na mikopo ambayo serikali ya China kutoa kwa nchi zote duniani na Waziri Makamba alikwenda kufanya mazungumzo na mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayoendelea nchini China.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad