HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 26, 2024

RUVUMA:JESHI LA POLISI WAMTIA MBARONI WIZI WA VIFAA NDANI YA MAGARINI HALFA MINJA MKAZI WA SANAWALI JIJI LA ARUSHA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya,akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jana wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watu mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya uharifu mkoani humo.
 Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi mwandamizi Marco Chilya,akiwaonyesha Waandishi wa Habari(hawapo pichani)baadhi ya milipuko(baruti) aina ya Super Powder 90 zenye vipande 12 kila moja iliyokamatwa na Jeshi hilo kutoka kwa mkazi wa mtaa wa Hoa Hoa wilayani Mbinga Edmund Komba(34) ambaye alikutwa na Dazeni mbili za milipuko hiyo kinyume cha sheria
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya,akionyesha baadhi ya kompyuta Mpakato(Laptop)zilizokamatwa na Polisi kutoka kwa kinara wa wizi ya vifaa vya ndani ya magari mkazi wa Mtaa wa Sanawali Jijini Arusha Halfa Minja,kukatamtwa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na operesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali mkoani humo.


Na Mwandishi wetuRuvuma
KAMANDA  wa Jeshi la polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya amesema,wanawashikilia watu watatu akiwemo mkazi wa mtaa wa Sanawali Jijini Arusha Halfa Minja kinara wa wizi wa vifaa ndani ya magari mkoani humo.

“Kwa muda mrefu Minja amekuwa akijihusisha na matukio ya kuvunja vioo vya magari na kuiba vifaa anavyovikuta ndani ikiwemo Laptop,tunaendelea kumshikilia yeye na wenzake wawili kwa ajili ya uchunguzi na mara upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani”alisema.

“tumebaini na kujua mtandao wote wa watu wanaojihusisha na wizi wa vifaa kwenye magari kuanzia wavunjaji,wasafirishaji na wanaopokea vifaa hivyo ambao wako Dar es slaam”.

Aidha alisema,wamemshikilia mkazi wa mtaa wa Hoahoa wilayani Mbinga Edmund Komba(34) akiwa na Dazeni mbili za milipuko(baruti) aina ya Super Powder 90 zenye vipande 12 kila moja kinyume cha sheria.

Alisema,pamoja na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Jeshi hilo,lakini mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa wanaopata kutoka kwa raia wema na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Katika hatua nyingine Kamanda Chilya alisema,wamewakamata watuhumiwa 12 wa matukio makubwa yakiwemo ya ubakaji na wizi wa kutumia nguvu na silaha ambao tayari wamefikishwa mahakamani.

Chilya alisema,kati ya watuhumiwa hao,mmoja amehukumiwa kunyongwa hadi kufa,wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 kila mmoja kwa kosa la kubaka,wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kubaka na mmoja alikutwa na hatia ya unyang’anyi kwa kutumia silaha na amehukumiwa kwenda jela miaka 30.

Ametoa wito kwa raia wema, kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uharifu na waharifu ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria ili mkoa wa Ruvuma uendelee kuwa salama wakati wote.

Amewaomba wananchi wa mkoa huo kuepuka kujihusisha na biashara haramu ambazo ni kinyume cha sheria za nchi,badala yake, watumie muda wao kujikita katika shughuli halali za kuwaingizia kipato ambazo zitaleta tija kwa familia na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad