HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 3, 2024

JOKATE MWEGELO NI KIUNGO SAHIHI CHA UTENDAJI UVCCM.

Anaandika Humphrey Shao wa Msakuzi Kaskazini.

Kiongozi ni lazima awe ni yule anayejishughulisha kufikri kwa sababu ya watu na awe anaendana na watu anawaongoza, naona huu ndio Mtazamo uliomuongoza Dkt.Samia Suluhu Hassan kumchagua Mdada Mtanashati Ndugu Jokate Urban Mwegelo kuongoza Jumuiya ya Vijana.

Jokate ambaye anashika nafasi hiyo miezi michache akiwa ametokea katika Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ambapo kwa muda mchache alikuwa amekaa huko ameweza kuleta mageuzi Makubwa ya kiutendaji na hiyo ndiyo kazi kubwa ya kiongozi kwani kila unapopatiwa kazi lazima uhakikishe unaacha alama katika kipande unachopewa kuongoza.

Jokate Mwegelo mtu wa maana sana na mtu bingwa ambaye ameweza kufanya mabadiliko makubwa katika kila kipande alichopewa kuongoza tangu alivyoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambapo aliondoka katika Wilaya hiyo kwenda kupangiwa majukumu mengine angali bado watu wa Kisarawe wanamuhitaji.

"Ni kweli kabisa kwamba kila mtu aliye mzima kiafya anaweza kutenda lakini si kila mtu anaweza kujenga fikra zenye mantiki zinazoweza kuzaa falsafa za maendeleo kwa watu anawaongoza" alisema Mama yangu mzazi na kusema kuwa hakika binti huyu falsafa zake zina akisi maendeleo ya kweli.

Rais anapochagua kiongozi maana yake anachagua mtu atakayekuwa anafikri kwa niaba yake na kuwa daraja la kutatua matatizo ya wananchi na siyo mtu atakayekuwa anafikri kwa niaba yake binafsi kama ambavyo tunaona wanasiasa wengi lakini Ndugu Jokate mara zote amekuwa akifikiri kwa niaba ya wengine.

Watanzania hasa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wanapaswa kumshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea kiongozi huyu mchapakazi na Mwadilifu.

Hivyo Mimi kama kijana kutoka Mtaa wa Msakuzi Kaskazini Mbezi Jijini Dar es Salaam niendelee kumpongeza Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana Ndugu Jokate Urban Mwegelo kwa kuaminiwa tena katika majukumu haya mapya kwani hapa sasa ndio sehemu sahii kwake kuonesha kile kilichobaki kwa Watanzania na kuwaongoza Vijana katika njia iliyonyooka.

Kipekee nitoe Shukrani zangu za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kutuamini Vijana katika majukumu ya kitaifa


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad