HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 3, 2024

ATE YAZINDUA MPANGO WA ELIMU YA UONGOZI KWA WANAWAKE


Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Susanne Ndomba na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Benard Kavishe wakionesha mkataba wa makubaliano jijini Dar es Salaam wa kuwadhamini wanawake 42 kupata mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 3,2024. 

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Susanne Ndomba na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Benard Kavishe wakisaini mkataba wa makubaliano jijini Dar es Salaam wa kuwadhamini wanawake 42 kupata mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 3,2024.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Susanne Ndomba na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Benard Kavishe wakibadilishana mkataba wa makubaliano jijini Dar es Salaam wa kuwadhamini wanawake 42 kupata mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha miaka mitatu. Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 3,2024.

 Mkurugenzi Mtendaji wa  Impact Leadership Academy (ILA), Zuhura Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa mpango wa uongozi kwa mwanamke utimiza miaka kumi tangu kuanzishwa.

Baadhi ya washiriki wa mpango wa uongozi kwa mwanamke.

CHAMA cha Waajiri Tanzania kimezindua kikundi cha kumi cha mpango wa malengo ya wanawake (FFP) ili kuwawewezesha wanawake na kuwapa ujuzi wa uongozi kwa nia ya kuweka usawa wa kijinsia katika sekta zote nchini.

Hayo yamesemwa leo Aprili 2, 2024 jijini Dar es Salaam na na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji wa ATE , Susanne Ndomba ambapo amesema mpango wa uongozi kwa mwanamke utimiza miaka kumi tangu kuanzishwa.

"Mbali na uzinduzi huo, pia tumetia saini Mkataba wa makubaliano na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania( ERB), ambao wamejitolea kuleta wanafunzi 13 wa kike kila mwaka kutoka katika taasisi zake ili kushiriki katika mpango huo.

" Hii inatuthibitishia usahihi wa kile tunachofanya . Pia unaweza kuona tofauti kwani katika kundi la tisa tulikuwa na wahitimu 76 mwezi uliopita, lakini katika kundi hili jipya, jumla ya wanawake 116 kutoka kampuni 27 wamejiandikisha mpaka kufikia jana,” amesema.

Amesema, mkataba kati ya ATE na ERB utadumu kwa miaka mitatu ambapo ERB inatarajiwa kuwekeza kiasi cha Dola za kimarekani 39000 kwa wanawake 13 huku ATE ikitoa nafasi moja ya bure kila mwaka kwa mtu mmoja kuhudhuria programu bila wao kulipa. "Tunafanya hivi ili kuvutia watu wengi zaidi kuhudhuria katika siku zijazo"amesema Ndomba.

Amesema mpango huo umekuwa na mtazamo chanya na kuvutia kampuni nyingi kwani unatoa mafunzo kwa wanawake katika maeneo ambayo kampuni hizo zimekuwa yakiwekeza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wanawake.

"Mpango huu unafunza wanawake katika maeneo matatu muhimu, ambayo ni: umahiri wa bodi, ustadi wa Uongozi na uweledi katika mawasiliano. Madhumuni ya programu ya baadaye ya wanawake ni kutoa na kuendeleza ujuzi wa wanawake kwa miezi tisa, "amesema.

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Mhandisi Benard Kavishe amesema juhudi za kuwawezesha wanawake ni muhimu ili kuwainua wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo ya nchi.

"Tuko hapa kama sehemu ya juhudi za kupigania usawa wa kijinsia haswa katika sekta ya uhandisi. Uhandisi ni miongoni mwa sekta ambazo zinaongozwa na wanaume. Katika kila wahandisi watano, kuna mwanamke mmoja tu. Idadi ndogo ya wahandisi wa kike katika sekta hii ni tatizo kubwa. Na kama ukirejelea malengo ya maendeleo ya milenia na malengo ya maendeleo endelevu, ni wazi kuwa kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia ni ishara ya maendeleo duni,” amesema.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Global Compact Tanzania, Masha Makatayambi amewapongeza viongozi hao kwa mpango huo wa kufungua milango kwa wanawake kushiriki katika mpango huo.

“Wanawake wana mahitaji mbalimbali yanayotofautiana na wanaume. Kupitia mpango kama huo usawa wa kijinsia unaweza kufikiwa programu hizi zitawachochea viongozi wa kiume kuiga mfano wa kutetea uwezeshaji wa wanawake, uamuzi ambao utatoa matokeo chanya kitaifa na kimataifa,” amesema.

Makatayambi, amesema mengi yanahitajika ili kukabiliana na idadi ndogo ya viongozi wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad